Breaking News

BRELA WAKUTANA NA WADAU WAJADILI RASIMU YA MKATABA WA SHERIA KIMATAIFA YA WIPO

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Godfrey Nyaisa akifafanu jambo katika warsha na wadau kutoka taasisi mbalimbali iliyolenga 
kujalidili na kupata maoni juu ya Rasimu ya Mkataba wa Sheria ya Kimataifa inayohusu Ulinzi wa Maumbo Bunifu na Michoro jijini Dar es Salaam.

Dar es salaam:
Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wamekutana na wadau kutoka taasisi mbalimbali  kwa lengo la kujalidili na kupata maoni juu ya Rasimu ya Mkataba wa Sheria ya Kimataifa inayohusu Ulinzi wa Maumbo Bunifu na Michoro.

Akizungumza katika warsha hiyo Ofisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Godfrey Nyaisa amesema 
maoni hayo watayawasilishwa katika mkutano wa Kideplomasia wa nchi Wananchama wa Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO) ambapo Tanzania ni mwanachama.

"Maoni haya yatayawasilishwa katika mkutano wa Kideplomasia wa nchi Wananchama wa Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO) ambapo Tanzania ni mwanachama ambao unatarajiwa kufanyika Riyadh nchini Saudi Arabia kuanzia Nov. 11 hadi 22 mwaka huu". Alisema Bw. Nyaisa.
Alisema endapo sheria hiyo itapitishwa na Tanzania kuridhia ni dhahiri itatoa fursa na kuongeza wigo kwa wabunifu wa maumbo, michoro bunifu ya Kitanzania kwa kuzisajili na kulinda kazi zao katika ngazi ya kimataifa na kukuza biashara zao jambo litakalosaidia kuweza kuhimili ushindani katika masoko ya ndani na kimataifa.

Bw. Nyaisa aliongeza kuwa kulingana na ushindani uliopo wa kinachotakiwa kwa watanzania kuongeza ubora wa bidhaa, huduma na muonekano kuanzia kwenye bidhaa husika, vifungashio, mikebe kwa lengo la kuongeza thamani na itasaidia kuwa rahisi kutambulika na kuvuta wanunuzi.

Kwani Mkataba wa WIPO wa Sheria ya Maumbo Bunifu unalenga kuweka utaratibu au mfumo wa Kimataifa wa Usajili na Ulinzi wa Maumbo Bunifu kwa nchi na Mashirika Wanachama, mfumo huu utawezesha uwasilishaji wa maombi ya ulinzi wa maumbo bunifu kupitia WIPO ambapo mwombaji ataweza kuwasilisha ombi moja na kuchagua nchi zaidi ya moja zitakazokuwa zimeridhia mkataba huo ambazo anahitaji kupata ulinzi wa ubunifu wake.

Alisisitiza katika kuhakikisha watanzania wanafanya vizuri BRELA imejipanga kuendelea kutoa elimu kwa wajasiriamali na wabunifu ili waweze kufanya bunifu zitakazowawezesha kutambulika kirahisi sokoni na kuhimili ushindani.
“Ili kuhakikisha elimu ya masuala ya Miliki Bunifu inawafikia wadau wengi tumejipanga kutashirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Shirika la Miliki Kanda ya Afrika (ARIPO) kutoa mafunzo kwa wakufunzi, Novemba mwaka huu kwa lengo la kupata idadi kubwa ya wakufunzi ambao watatoa elimu kwa wajasiriamali lukuki hapa nchini na kuhakikisha, Miliki Bunifu inakuwa chachu ya maendeleo ya kukuza uchumi kama ambayo nchi zilizoendelea zinafanya,”
 Alisema Bw. Nyaisa

Kwa upande wake bwana Mustafa Haji, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa BPRA, bwana Khamis Juma Khamis, amesema vikao kama hivyo ni vema pia kikafanyika Zanzibar kwa lengo la kuendelea kushirikiana kwa maslahi ya taifa kwa ujumla.

Naye Mhadhiri kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambaye pia ni Meneja wa Miliki Bunifu Dokta Perfect Melkiori amesema kumekuwepo na changamoto kubwa kwa wanafunzi na wafanyakazi kutojua thamani ya bunifu zao jambo linalopelekea kurubiniwa na baadhi ya kampuni na mashirika ili kuuza bunifu zao kwa bei ndogo.

"Kumekuwepo na changamoto kubwa ya kutokuwa na uelewa juu ya bunifu hivyo ipo haja kujikita zaidi kutoa elimu ili kuhakikisha kundi hilo halipotezi haki ya kwa kuuza bunifu kwa gaharama ndogo kutokana na kurubuniwa na kampuni na mashirika". Alisema Dkt Melkiori.



No comments