Breaking News

EXTRA POWER SKIMMING PUTTY YAWATAMBULISHA ALLY KAMWE NA AHMED ALLY KUWA MABALOZI WA BIDHA ZAO

Mkurugenzi wa kampuni ya skimming Putty bwana Hamoud Shabiby akizungumza katika hafla ya kuwatambulisha mabalozi wapya wa bidhaa ya simenti ya Extra Power Skimming putty Msemaji wa Klabu ya Simba Ahmed Ally na Msemaji wa klabu yanga Ally kamwe katika hafla iliyofanyika katika hotel ya Serena Jijini Dar es salaam.
Msemaji wa Klabu ya Simba na balozi wa kampuni ya Extra Power Skimming, bwana Ahmed Ally akifafanua jambo mara baada ya kutambulishwa kuwa balozi mpya wa Extra Power Skimming hafla iliyofanyika katika hotel ya serena Jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa yanga na balozi wa kampuni ya Extra Power Skimming Ally kamwe akiongea mara baada ya kutambulishwa kuwa balozi mpya wa Extra Power Skimming hafla iliyofanyika katika hotel ya serena Jijini Dar es Salaam.

Dar es salaam:
Kampuni ya Rockmax imewatambulisha wasemaji wa club kongwe za mpira wa miguu nchini Simba na Yanga Ally Kamwe na Ahmed Ally kuwa mabalozi wa bidhaa ya simenti ya Extra Power Skimming putty.

Akizungumza katika hafla ya kuwatambulisha mabalozi hao wapya katika hotel ya serena Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa kampuni ya skimming Putty bwana Hamoud Shabiby amesema lengo la kampuni hiyo imeingia makubaliano na wasemaji hao kuwa mabalozi wa bidhaa zao ni kutokana na ubora wa wa bidhaa yao inayoongoza Afrika Mashariki.

"Bidhaa yetu ya Cement Extra power imepokelelewa vizuri kwa mafundi na wajenzi wa nyumba, ambapo katika kila mfuko wa Extra Power skimming wa kutakuwa kuponi ya shilingi 2000 itakayomuwezesha mtumiaji kutumia kwenye simu yake kama vocha uu Salio la M-pesa, Au Tigo pesa". Alisema Bw. Shabiby.

Nae Msemaji wa Klabu ya Simba na balozi wa kampuni ya Extra Power Skimming, bwana Ahmed Ally amesema kupitia kampuni hiyo imetoa fursa muhimu kwa kijana ambaye amewekeza na kuajiri vijana wengi wa kitanzania.

"Kampuni Extra Power Skimming pamoja na kurudisha kwa jamii sehemu ya mapato yake imetoa fursa muhimu kwa kijana ambaye amewekeza na kuajiri vijana wengi wa kitanzania". Alisema Bw. Ahmed Ally.

Kwa upande wake Msemaji wa yanga na balozi wa bidhaa hiyo, bwana Ally kamwe amesema Hadi kukubali kuwa Balozi wa bidhaa hiyo bora nchini tayali nimejiridhisha kuhusu ubora bidhaa hiyo hasa katika suala la ujenzi.

"Napenda kuchukua nafasi hii kutoa wito kwa mafundi na wateja wengine kutumia bidhaa hii ya Extra Power Skimming putty kwani ni bora ya bidhaa ye ye viwango vya hali ya juu". Alisema Ally kamwe.

Alisema vijana wengi nchini wamekuwa na mwako mkubwa wa kuachana na maisha ya kununua magari na kuibukia kwenye ujenzi. 

No comments