Breaking News

ACT YATANGAZA MAADHIMIO YA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU, YARIDHIA KUSHIRIKI UCHAGUZI SEREKALI ZA MITAA

Na Neema Mpaka
Chama cha  ACT Wazalendo kimesema kimejiandaa kushiriki kikamilifu katika Uchaguzi wa serikali za mitaa unatarajiwa kufanyika Novemba 27 Mwaka huu.

Akizungumza na waandishi wa Habari makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam, Naibu katibu Mwenezi Bi. Shangwe Ayo amesema chama kitasimamisha wagombea katika ngazi zote za vitongoji na mitaa.

"Halmashauri kuu ya Chama iliyoketi siku mbili Agoust 24 na 25 imepokea na kujadil taarifa mbalimbali ikiwemo ya maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za mitaa pamoja na program za Ujenzi wa chama ikiwemo mikutano ya Hadhara na kuhadhimia kwa kauli moja kusimamisha wagombea" Alisema Shangwe Ayo.

Bi. Shangwe aliongeza kuwa chama  kimepokea progamu ya miezi 10 ya kuendesha mikutano ya Hadhara katika maeneo mbalimbali ya Tanzania bara na Zanzibar na kufanikiwa kuvuna wanachama wapya katika  kipindi hichp cha miezi 10. 

No comments