Breaking News

WAZIRI UMMY AMWKILISHA RAIS DKT. SAMIA NCHINI ETHIOPIA

Na. WAF, Ethiopia.
WAZIRI wa Afya Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb) ambaye pia ni Mjumbe Maalum wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan amewasilisha rasmi ujumbe maalum wa Rais Dkt Samia kwa Rais wa Jamhuri ya Watu wa Ethiopia Mheshimiwa Sahle-Work Zewde, Julai 8,2024.

Waziri Ummy pamoja na wajumbe wake amekabidhi rasmi ujumbe maalum kwa Mheshimiwa Sahle - Work Zewde, Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ethiopia jijini Addis Ababa Ethiopia.
Akipokea salaam hizo, Rais wa Ethiopia aliishukuru Tanzania kwa ushirikiano mzuri Katika nyanja mbalimbali  ambao ulianzishwa na Waasisi wa Mataifa haya mawili

Kwa upande wake Waziri Ummy amemshukuru Rais  Sahle - Work Zewde kwa kutenga muda wake na kupokea ujumbe maalum wa Rais Dkt .Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


No comments