Breaking News

WAZIRI KAIRUKI AWATAKA WANANCHI KATAVI KULINDA MAENEO YA HIFADHI

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amewataka wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe, Mkoani Katavi kulinda maeneo ya hifadhi na kuacha kufanya shughuli za kibinadamu katika maeneo hayo.

Ameyasema hayo leo Julai 15,2024 wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo Mkoani humo.
"Tuyalinde mapori yetu ya akiba, na tusifanye shughuli za kilimo na ufugaji kwenye maeneo yaliyohifadhiwa" amesisitiza Mhe. Kairuki.

Mheshimiwa Kairuki yupo katika ziara ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye yupo mkoani Rukwa kwa ziara ya kikazi.

No comments