Breaking News

TANESCO: MABORESHO YA LUKU MIKOA YA DAR NA PWANI KUANZA JULAI 22, 2024

Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Bi. Irene Gowelle akifafanua jambo katika mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam:
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limesema linatarajia kuanza kufanya maboresho ya mfumo wa luku kuanzia Julai 22, 2024.

Hayo yamebainishwa leo Julai 15, 2024 na Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma TANESCO Irene Gowelle akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salama.

Amesema kuwa katika maboresho hayo ni kwamba wakati mteja atakaponunua umeme kwa mara ya kwanza atapokea tarakimu kwenye makundi matatu ambapo kila kundi litakuwa na tarakimu 20.

Hivyo ametumia fursa hiyo kuwataka wateja wake wa Mkoa wa Dar es Salaam na Pwani kufanya maboresho hayo yatakapoanza kwani lengo la kuendana na mabadiliko ya mfumo wa mita za luku ya Kimataifa pamoja na kuongeza ufanisi na usalama.
Bi. Gowelle ameongeza kuwa kundi la kwanza na pili la tarakimu litakuwa kwa ajili ya maboresho ya mfumo wa luku, huku kundi la tatu kwa ajili ya umeme utakaokuwa umenunuliwa na mteja.

“Mteja ataingiza umeme tarakimu za kila kundi katika luku yake kwa mfatano unaosomeka kwenye risiti ya malipo au ujumbe mfupi wa maandishi (sms) na kila utakapoingiza kundi moja mteja anapaswa kubonyeza alama ya kukubali ya # au msale wa kukubali na hapo utakuwa umefanikiwa kuboresha mita yako na kupokea kiwango cha umeme ulionunua” amesema Gowelle na kuongeza,

"Wateja ambao watashindwa kufanya maboresho ya luku mpaka kufikia Novemba 24, 2024 watakosa huduma ya umme hadi wakapofika katika ofisi za TANESCO kwa ajili ya kupata msaada wa maboresho ya mfumo wa luku,". 

Gowelle ameeleza kuwa TANESCO wajipanga katika mikoa yote kwa ajili ya kuwasaidia wateja wakati wanapopata na changamoto katika kipindi chote cha maboresho ya mita za luku.

“Zoezi la maboresho ya luku ni bure na litafanyika mara moja kwa kila mteja na baada ya kufanya hivyo atakuwa amefanya maboresho na ataendelea kupata kundi moja la tarakimu 20 kila atakapofanya manunuzi ya umeme” ameeleza Gowelle.

Amesema kuwa baada ya mikoa ya Kusini na Kanda ya Nyanda za juu kusini zoezi kukamilika, litaendelea kwa mikoa mingine nchini kwa awamu kadri Shirika la TANESCO litakavyotangaza kwa umma, huku akibainisha kuwa mwisho wa zoezi hilo nchini ni Novemba 24, 2024.

Ameeleza kuwa endapo mteja atakutana na changamoto wakati anafanya maboresho ya mita za luku atawasiliana na Mkoa husika wa Kitanesco kupita namba : Mkoa wa TANESCO Temeke – 0694 169 798, Ilala – 0733 212 575, Kinondoni Kusini – 0756 251 753, Kinondoni Kaskazini – 0692 7685 87, Pwani – 0738 256 237.

Kampeni ya maboresho ya mita za Luku imebeba kauli mbiu inayosema ‘Mita yako tunakazi nayo’. 

No comments