Breaking News

WAKAZI WA MATUGA NA MTEGO WA SIMBA WALIA NA UONEVU UNAOFANYWA NA HALMASHAURI YA MJI WA KIBAHA

Wakazi wa maeneo ya Matuga na Mtego wa simba mkoani Pwani wamemwomba waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya makazi Jerry Silaa kuingilia kazi kwa kile walichokiita kuwa ni uonevu unaofanywa na halmashauri ya mji wa kibaha kwa kubomoa nyumba zaidi ya 700 zilizokuwa katika maeneo hayo mwezi Februari 2023.

Akizungumzia sakati hilo wananchi hao wamesema pamoja na shauri hilo kupelekwa mahakama kuu kitendo cha ardhi na kushinda kesi bado halmashauri ya mji ya kibaha imekuwa ikifanya vitendo vya uonevu mbalimbali ikiwemo kuwakamata wananchi ma kiwaweka rumande 

"Sisi wakazi wa eneo hili la Matuga na Mtego wa simba mkoani Pwani mara naada ya kufungulia kesi na tukashinda kwa ushindi mkuu, lakini pamoja na ushindi tulioupata mahakamani bado Halmashairi hiyo inatusumbua kwa kumkamata mtu mmoja mmoja na kumsotesha rumande na wakati mwingine wanakuja na askari huku wakitoa vitisho wakiwa na siraha za moto". Walisema 
Walisema halmashauri ya mji wa kibaha umekuwa ukipima maeneo ya watu ambayo hususani waathirika ambao hawakufanikiwa kurejea katika viwanja vyao kutokana na kuathirika kiuchumi kisha kuviuza.

Waliongeza kuwa mapema wiki iliyopita Tunamshukuru Waziri wa Ardhi Mhe. Jerry Silaa alifika katika eneo husika na kutoa maelekezo kadhaa cha kushangaza mara baada ya kuondoka waziri halmashauri iliendelea na vitendo walivyoviita kupuuza maagizo hayo apuuza kwa kutesa wananchi wenzetu walioweza kurejea katika maeneo yao kwa kuanza kujijenga upya na wengine kulala nje

"Tunamshukuru Waziri wa Ardhi Mhe. Jerry Silaa kwa utayali wake na kufika eneo husika wiki iliyopita pamoj na kutoa maelekezo kadhaa
lakini mara baada ya kuondoka kwa mheshimiwa waziri, halmashauri ndio kwanza kama wanaongeza hasira zao kwani wamekuwa  wakiwatesa wananchi wenzetu walioweza kurejea katika maeneo yao kwa kuanza kujijenga upya na wengine kulala nje". Alisema 

"Tunaomba ndugu waandishi wa habari mtusaidie kupasa sauti kilio kikubwa na mateso tunayopitia pamoja na kushinda kesi mahakamani lakini hata ushindi wetu wa awali kule mahakamani ulisababishwa na sauti yetu mlipopaza sauti juu ya mgogoro huu februari 2023".

No comments