Breaking News

VIONGOZI WA DINI TUWAFUNDISHE VIJANA MAFUNDISHO YA DINI - DKT. SAMIA

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa Dini zote kukaa na kufundisha Vijana kufuata mafundisho ya Dini akisema Watu waliopitishwa kwenye mafunzo ya Dini hawawezi kusimama wakanyanyua midomo kuwatusi au kuwakashfu Viongozi wao.

Rais Samia ameongea hayo Visiwani Zanzibar leo July 05,2024 wakati akishiriki Kongamano la Wanawake wa Kiislamu, ambapo yeye ndio Mgeni rasmi ambapo amesema “Wakati mwingine nikisoma kwenye mitandao ya kijamii, nikisikiliza hotuba za Wanasiasa wenzetu jinsi wanavyowachambua na kuwadhalilisha Viongozi wetu napata mashaka kama kweli tumepata malezi ya kiimani au kwetu Dini hii tunaifanya kama utamaduni tu au mila bila kufuata na kuwa na imani ya kweli na Dini yetu”.
“Nimekuwa nikisema mara kadhaa kwamba Watu waliopitishwa kwenye mafunzo ya Dini hawezi kusimama akanyanyua mdomo akamtusi au akamkashifu Kiongozi wake hawezi, kwahiyo wale wanaofanya ni kwasababu hawakupita kwenye malezi ya kidini, na wito wangu huwa nasema na Viongozi wa Dini zote kukaa na kufundisha Vijana wetu”

“Majukwaa ya Siasa yana hamasa, yana ashiki, yanashawishi Mtu akikaa kwenye jukwaa basi yanamtoka tu, tuongeze jitihada kwa Vijana wetu, kwa Watu wetu tuwe na milimi laini”.



No comments