Breaking News

TANESCO YATOA UFAFANUZI MAKATO KWENYE LUKU

Baada ya wateja kulalamika kuhusu makato ya Sh. 2,000 kwenye LUKU, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), limesema hakuna ongezeko la Kodi ya Majengo isipokuwa pesa hizo zimekatwa kufidia madeni yaliyotakiwa kulipwa 2023/24.

Taarifa ya TANESCO ilieleza, hatua hiyo inatokana na mabadiliko ya Kodi yaliyotangazwa Julai 26, 2023 na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kutoka Sh. 1,000 hadi 1,500 na Sh. 5,000 hadi Sh. 7,500 ambapo makato hayo yanawahusu walionunua Umeme kati ya Julai Mosi hadi 25, 2023 na walikatwa Sh. 1,000 badala ya Sh. 1,500 au Sh. 5,000 badala ya Sh. 7,500.

Aidha, TANESCO ilisema makato hayo yamefanyika mara moja kwasababu yalitakiwa kulipwa kupitia ununuzi wa Umeme kwa wadaiwa wote wanaonunua huduma hiyo kuanzia Julai Mosi, 2024.

No comments