Breaking News

SHEIKH JALALA AWATAKA WAISLAM KUYAISHI NA KUENZI MATENDO YA IMMAM HUSSEIN {A.S}

Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna'ashariyyah Tanzania T.I.C Sheikh Hemedi Jalala Mwakindenge akizungumza katika Matembezi ya Amani leo tarehe 17/07/2024 sawa na 10/ Muharram 1446H ya  kumbukumbu ya kifo cha Swahaba na Mjukuu wa Mtume Muhammad s.a.w.w Al-Imam Hussein a.s aliyeuliwa katika Ardhi ya Karbalaa- Iraq mwaka 61H.l  jijini Dar es saalam.
Mwenyekiti wa wanawake Jumuiya ya Shia Ithna'ashariyyah Tanzania T.I.C Taifa, Fatuma Ally Mwuru akizungumza katika Matembezi ya Amani ya kumbukumbu ya kifo cha Swahaba na Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) Al-Imam Hussein a.s aliyeuliwa katika Ardhi ya Karbalaa- Iraq mwaka 61H.l jijini Dar es saalam.

Dar es Salaam

Waumini wa dini ya kislam nchini watakiwa kuendelea kudumisha Amani, umoja na mshikano uliopo hili kuweza kutunza tunu hiyo ambayo ni adhimu ikiwa ni pamoja na kumuenzi mafundisho na matendo ya Imam Hussein A.S

Akizungumza katika Matembezi ya Amani leo tarehe 17/07/2024 sawa na 10/ Muharram 1446H Mkuu wa Jumuiya ya Shia Ithna'ashariyyah Tanzania (T.I.C} Sheikh Hemedi Jalala Mwakindenge amesema kumbukumbu ya kifo cha Swahaba na Mjukuu wa Mtume Muhammad s.a.w.w Al-Imam Hussein a.s aliyeuliwa katika Ardhi ya Karbalaa- Iraq mwaka 61H.

Alisema tukiwa tunakumbuka kumbukumbu ya kifo cha Swahaba na Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w_ Al-Imam Hussein a.s ni vema kuendelea kuishi na kuyafata mafundisho yote ambayo amekuwa akiyaishi kipindi chote cha uhai wake.

"Leo Kupitia matembezi ya Amani tunakumbuka kifo cha Swahaba na Mjukuu wa pili wa mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w) Al - Imam Hussein A.S aliyeuliwa katika Ardhi ya Karbalaa - Iraq mwaka 61H yawe chachu kwa kuendeleza Amani, Umoja na Mshikamano" Alisema Sheikh Jalala.

Aidha sheikh Jalala pia ametoa pongezi kwa rais Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo amekuwa akiongoza na hatua ambazo amekuwa akizichukua kuhakikisha amani, Umoja na mshikamano vinaendela kuwepo tangu ameingia madarakani.

"Nitoe rai kwa waumini wa dini ya kiislamu kuendelea kuiombea serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia amefanya kazi kubwa ya hasa katika kuhakikisha kuwa amani, umoja na mshikamano vinaendelea kudumishwa nchini". Alisema Sheikh Jalala


Matembezi ya Amani ya kumbukumbu ya kifo cha Swahaba na Mjukuu wa Mtume Muhammad (s.a.w.w) Al-Imam Hussein a.s aliyeuliwa katika Ardhi ya Karbalaa- Iraq mwaka 61H.l jijini Dar es saalam.

No comments