Breaking News

ACT WAZALENDO WALAANI KAULI YA WAZIRI NAPE

Chama cha ACT Wazalendo kimelaani kauli iliyotoleaa na waziri wa habari mawasailiano, Nape Nnauye kufatia kusambaa video katika mitandao ya kijamii kuwa uchaguzi matokeo ayatokani na kura pekee zitakazopigwa.

Akizungumza mapema leo Julai 17, 2024 makao makuu ya chama hizo jijini Dar es salaam Naibu Katibu wa Idara ya Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma, Shangwe Ayo amesema chama kinalaani kauli hiyo pamoja na kuichukulia kwa umakini mkubwa kufatia kuelekea katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwishoni mwa mwaka huu na uchaguzi mkuu ujao wa rais na wabunge.

Katika hatua nyingine Bi. Shangwe Ayo alibainisha kuwa chama kimepanga kuanza ziara ya kitaifa katika mikoa 22 na majimbo 125 ya Tanzania Bara lemge lengo la kujiandaa kuelekea uchaguzi ujao wa serikali za mitaa unaotarajiwa kufanyika baadaye mwaka huu na uchaguzi mkuu mwakani.

Alisema ziara hiyo itaanza rasmi Julai 22 ambapo Kiongozi wa chama hicho Dorothy Semu katika katika mikoa 30 ambayo ni Arusha, Kilimanjaro, Dodoma, Singida na Manyara na Makamu Mwenyekiti wa chama bwana Isihaka Mchinjita ataelekea katika majimbo 38 mikoa ya Ruvuma, mkoa wa kichama wa Selous, Mtwara, Lindi, Pwani na Tanga

Alisema katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa ACT Wazalendo Ado Shaibu yeye atatembelea majimbo 21 katika mikoa ya Mwanza, Simiyu, Mara, Geita na Kagera.

Aliongeza kiwa nae Kiongozi mstaafu wa chama hicho Zitto Kabwe yeye atatembelea majimbo 36 katika mikoa ya Kigoma, Rukwa, Katavi, Tabora, mkoa wa kichama Kahama na Shinyanga

Bi. Ayo alisema katika ziara hiyo chama kinataraji kuzindua mpango wa kusajili wanachama wapya milioni 10 ndani ya kipindi cha miezi 10 kuanzia mwezi Julai 2024 na Aprili 2025, sambamba na hilo viongozi hao wanatarajia kuwahamasisha Watanzania kujiandikisha kuwa wapiga kura kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa (2024) na uchaguzi mkuu (2025) wakilenga kuona chama hicho kinapata ushindi wa kishindo kwenye chaguzi hizo

"Kupitia ziara hii viongozi wakuu wa ACT Wazalendo wanakusudia kusikiliza kero mbalimbali za wananchi zinazohusu masuala ya kiuchumi, kijamii na kisiasa ili wazipazie sauti na kuendelea kuinadi ahadi ya chama hicho kwa Watanzania ya kujenga ‘Taifa la wote, maslahi ya wote" Alisema Bi Shangwe Ayo

No comments