Breaking News

NSSF: WATUMISHI MNAOTARAJIA KUSTAAFU HAKIKINI TAARIFA ZENU

Mfuko wa Taifa wa hifadhi ya jamii (NSSF) umewataka watumishi wanaotarajiwa kustaafu kuanza kujiandaa ikiwa ni pamoja na kuhakiki taarifa zao za msingi sambamba na kuwa na nidhamu ya matumizi ya fedha hali itakayosaidia kupunguza changamoto za maisha pindi wanapostaafu 

Rai hiyo imetolewa jijini Dar es salaam na meneja wa mafao wa NSSF Ilala, wakati akimuwakilisha mkurugenzi wa uendeshaji bwana Mrisho Mwisimba wakati akifungua warsha iliyolenga kutoa elimu kwa watumishi wanaotarajia kustaafu kutoka katika mkoa wa Temeke ambapo pia amewasisitiza watumishi hao pia kuanzisha miradi salama ya uwekezaji ili kuwa na uhakika wa kipato endelevu.

"Nitoe rai kwa watumishi wote hususani mnaotarajia kustaafu kuhakiki taarifa zenu mapema kwani kwa kufanya hivyo itasaidia kuepuka changamoto mbalimbali ambazo zinaweza kujitokeza pi di watakapostaafu". Alisema Bw. Mwisimba.
Kwa upande wake Emmanuel Nyange meneja idara ya biashara kutoka benki ya biashara ya taifa (TCB), ambao pia walihudhuria mafunzo hayo kwa ajili ya kutoa elimu ya fedha katika mafao amesema kuwa, TCB katika kipindi cha miaka 10 imekuwa ikishirikiana na wastaafu kwa ikijikita katika kutatua changamoto wanazokutana nazo pindi wanapostaafu kwa kuanzisha akaunti maalumu ya Kivulini isiyo na makato yeyote wala gharama za uendeshaji,lengo likiwa ni kumnusuru mstaafu.

"TCB katika kipindi cha zaidi ya miaka 10 tumekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimi ya fedha kwa watumishi wanaotarajia kustaafu pamoja na kushauri namna bora ya kujiandaa kuandaa miradi pamoja na kuanzisha account mahususi kwao ya kivulini isiyo na makati". Alisema Bw. Nyange

Aidha Bw. Nyange aliongeza kuwa Sambamba na hayo TCB Benki imeanzisha huduma za pesheni advance inayomuwezesha mstaafu kupata fedha ya kujikimu kwa kutoa suluhu kwa tatizo analokutuna nalo,ila pia kuna huduma ya mkopo usio na masharti yeyote  

Alisema kupitia akaunti ya kivulini TCB benki inatoa huduma za fixed akaunti hii mstaafu anaweza kupata mpaka asilimia asilimia 11 kwa mwaka, bado wastaafu wakipata majanga au ulemavu wa kudumu wanapewa fidia,na sababu kuu ni adhimio la serikali kuweza kufikia makundi yote katika huduma za ujumuishaji wa kifedha,
Huduma hizo zote zinatolewa katika mkitadha wa kutatua changamoto wanazopitia wastaafu hivyo kuwasihi wastaafu watarajiwa kuhakikisha wanasamehe na kuachana na yaliyopita na zaidi wafungue akaunti na tcb ili waweze kupata huduma zote hizo

Kwa upande wake Afisa Mafao mkuu wa NSSF Shakira Masoli amewasisitiza watumishi kujiandaa kustaafu kwa kuhakikisha wanapeleka na wanahakiki taarifa zote za msingi ili kuepusha usumbufu pindi wanapostaafu

"Pamoja na jitihada zote zinazotolewa na wadau ikiwemo TCB benk nipenda kuwasisitiza watumishi kujiandaa kustaafu kwa kuhakikisha wanapeleka na wanahakiki taarifa zote za msingi ili kuepusha usumbufu pindi wanapostaafu". Alisema Bi. Masoli.

Naye mmoja wa wanufaika wa NSSF, Bwana Damas Nungu ameutaka mfuko huo kupunguza kikokotoo cha awali anachopewa mstaafu huku akiwahimiza waajiri kupeleka michango ya watumishi wao kwa wakati. 

"Kwa dhati tunaotoa pongezi kwa mfuko wa Hifadhi ya jamii wa NSSF na TCB benki kwa kuwa nasi na kutupatia elimu juu ya mambo mbambali lakini pia napenda kutoa ombi kwa mfuko wa NSSF kuangalia namna ya kupunguza kikokotoo cha awali anachopewa mstaafu". Alisema Bw. Nungu

No comments