Breaking News

MRAMBA AIPONGEZA EWURA KWA UDHIBITI KWA UBORA

Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati Felchesmi Mramba amepongeza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji nchini (EWURA),

Akizungumza mara baada ya kutembelea banda la EWURA katika Maonyesho ya 48 Kimataifa ya sabasaba jijini Dar es Salaam amesema bei ya huduma husika ipo chini imeendelea kuwa stahamilifu yote ni kutokana na EWURA kuendelea kusimamia na kutoa huduma nzuri

Akizungumzia bei ya Umeme nchini ambapo hivi sasa ipo chini ukilinganisha na majira zetu wa jumuia ya afrika mashariki na hata Mataifa mengine afrika na Duniani,

"Wote mashahidi Ukiangalia bei ya Umeme wetu ipo chini sana tofauti na majirani zetu wa jumuia ya afrika mashariki Waandishi mnaweza kufatilia sababu ninyi mnaweza kufatilia kwenye Website(TOVUTI) za nchi Mbalimbali". Alisema Mhe. Mramba.

Alisema upatikamaji wa huduma ya Umeme hususani katika kipindi cha siku za hivi Karibuni umeimarika na changamoto ya kukatikakatika (MGAO) kwa sasa hakuna, hii inatokana na kuendelea kufanyika kwa maboresha mbalimbali ikiwemo kuongeza uzalizshaji na miundombinu ya kusambazia umeme. 

Akizungumzia juu ya upatikanaji na matumizi ya Gesi asilia Bw Mramba alisema EWURA imekuwa ikiendelea inatoa Leseni hasa kwa wale wanaojenga vituo vya (CNG), lakini pia EWURA inahakikisha ile huduma inayotolewa inakidhi viwango na mahitaji ya Jamii.

Aidha Bwana Mramba aliongeza kuwa Wizara ya Nishati itahakikisha kuwa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) inafanya kazi zake kwa mujibu wa sheria.
Nae Mkurugenzi wa EWURA, Bwana James Andilile amesema hivi Karibuni malmlaka hiyo imesaini mkataba na TANESCO kwa lengo la kusimamia utendaji kazi wao ili kuboresha utendaji na upatikanaji wa Umeme na kwa sasa Serikali inafanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya Nishati ili kuhakikisha sekta hiyo inaimalika zaidi.

Aidha Bw Andilile ametoa wito kwa wawekezaji wote wanaotaka kuwekeza katika sekta ya gesi nchini kujitokeza kwani gesi inapatikana hapa nchini ili kuwahudumia wananchi.

No comments