Breaking News

TANESCO YATOA HUDUMA KIDIGITALI YAWAPUNGUZIA WATEJA GHARAMA NA MUDA

Dodoma 
Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO),limetekeleza maagizo ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan ya kuyataka mashirika ya umma kujikita katika huduma za kidijitali kwa lengo la kuwarahisishia wananchi huduma.

Akizungumza leo Juni 19,2924 jijini Dodoma Afisa huduma kwa wateja wa Shirika hilo Fatuma Mohamed katika maonesho ya Wiki ya utumishi wa Umma ameeleza kuwa wameongeza wigo wa kutumia TEHAMA kwa upande wa kutoa taarifa mbalimbali ukiwamo wa JISOT.

"Tunaiita JISOT ni mfumo ambao mteja anaweza akatoa taarifa kwa njia ya simu janja kupitia namba yetu ile ile ya kutolea taarifa kwenye kituo cha miito ya simu TANESCO," amesema.

Ameeleza kuwa kwa kwa sasa mteja sio lazima afike ofisini ili kupata huduma ya kuonganishiwa umeme, mteja popote alipo akiwa na simu janja aunaunganishwa na mfumo wa NIKONECT ambapo atapata huduma kama ambavyo angefika katika ofisi za TANESCO.

Afisa huyo amefafanua kuwa mteja wa Shirika hilo akiwa na simu zile za kitochi anaweza kufanya maombi na anaweza kuonganishiwa umeme bila kufika ofisi za TANESCO.

Fatuma amesema faida ya huduma hizo ni kuokoa muda wa mteja kusafiri umbali pamoja na usumbufu wa kutafuta ofisi ili kujipatia huduma lakini pia TANESCO wameweza kupata taarifa kwa haraka kiganjani na urahisi wa kuhudumia mteja kwa uharaka.


No comments