Breaking News

DKT. KIJAJI KUFUNGUA MAADHIMISHO YA SEKTA YA MILIKI NA UBUNIFU DUNIANI

Waziri wa viwanda na biashara Dokta Ashatu Kijaji anatarajiwa kufingua maadhimisho ya siku ya miliki ubunifu Duniani kesho Mei 09 jijini Dar es salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Jijini Dar es salaam. Mkurugenzi wa Miliki Bunifu, Bi Loy Mhando amesema maadhimisho yalianzishwa na Shirika la miliki ubunifu Duniani (WIPO) yatawakutanisha wadau kutoka Taasisi za umma pamoja na sekta binafasi zinazosimamia miliki ubunifu.

"Maadhimisho ya siku ya Miliki Bunifu Duniani huadhimishwa kila mwaka Aprili 26 lakini kwa hapa kwetu kutokana na Tarehe hiyo kuwa na jambo muhimu la kitaifa la kuazimisha muungano sisi tunaazimisha siku tofauti ambapo mwaka huu tunaadhimishia tarehe 09 Mei 2024." Alisema Bi. Mhando.

Alisema maadhimisho hayo yataenda sambamba na matukio mbalimbali ikiwemo mijadala kuhusu Miliki Ubunifu ambayo itahusu fursa, mafanikio na changamoto wanazokutana nazo katika nyanja nzima ya miliki ubunifu.

Pia katika maadhimisho hayo hati za makubaliano ya ushirikiano katika eneo la Miliki Ubunifu baina ya BRELA ,COSOTA na Taasisi nyingine zitasainiwa ikiwa ni njia ya kurasimisha ushirikiano uliopo baina ya Taasisi hizo kuhakikisha sekta ya Miliki Ubunifu inaleta manufaa katika maendeleo ya kiichumi na teknolojia nchini.

Aidha bi. Mhando aliongeza kuwa Miliki Ubunifu inarija kubwa kwa wabunifu ambapo inawapa ulinzi wa kumiliki bunifu zao na kuwasaidia katika kupata haki zao endapo mtu yoyote ataingilia ama kutumia bunifu yake pasipo makubaliano na mmiliki.

Mashirika ya kimataifa na kikanda ya Miliki Ubunifu yaongeza wigo wa ulinzi wa bunifu za wabunifu katika maeneo mbalimbali Duniani hususani kwa wabunifu wa kazi zinazovuka mipaka