Breaking News

DKT SAMIA MGENI RASMI MAADHIMISHO MIAKA 85 YA KANISA LA TAG

Askofu Mkuu wa Kanisa Tanzania Asseblies Of God (TAG) Mchungaji Dokta Barnabas Mtokambali akifafanua jambo kwa waandishi wa habari juu ya maandalizi ya maadhimisho ya miaka 85 tangu kuanza kwa kanisa hili nchini. 

Dar es salaam 
Rais wa jamuhuri ya muungano wa TANZANIA dokta Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya miaka 85 tangu kuanzishwa kwa Kanisa la Tanzania Assemblie of God (TAG) nchini yatakayofanyika katika Uwanja wa Uhuru, Juni 14 jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia juu ya maandalizi ya maadhimisho hayo leo Mei  8, 2024 jijini Dar es Salaam Askofu Mkuu wa Kanisa hilo, Mchungaji Dkt Barnabas Mtokambali amesema dhima kuu ya maadhimisho hayo ni kumshukuru Mungu kwa uaminifu wake na kuwawezesha kubaki imara kama kanisa, taasisi kwa miaka 85.

“Maadhimisho haya ya miaka 85 itawawezesha kupokea kijiti na kumwishia Mungu katika zama hizi na zijazojili na aendelee kutenda makuu, pia kanisa la TAG limekuwa kielelezo cha ujenzi wa umoja, amani na upendo na kutoa huduma kwa jamii,”. Alisema Mtokambali.

Alisema maadhimisho hayo pia yanatarajiwa kuudhuliwa na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi wapatao 200, pia yanalenga kurithisha kwa kizazi kijacho imani ya kipentekoste kwa kuangalia namna watangulizi wao walivyotembea na Mungu na namna alivyowatunza na kutenda mambo ya ajabu.

Aidha Dkt. Mtokambali aliongeza kuwa katika kipindi cha miaka 85 kanisa limefanikiwa kueneza injili ya kristo kwa njia ya mbalimbali ikilenga kuleta mabadiliko chanya katika maisha ya watu na jamii kwa ujumla na kuongeza idadi ya washirika nchini kote.

Pia katika kipindi hicho Kanisa limefanikiwa kujenga vyuo tisa vya theolojia na uongozi wenye matawi 71 nchini kote jamnbo lililosaidia kuwekeza katika mafunzo, uongozi wa mfano na kusaidia kukuza viongozi wa leo na kesho.

Alisema katika miaka 85 ya huduma kanisa pia limefanikiwa kutekeleza agizo kuu na kuwezesha kuwa na wamisionari wa hapa nchini wanaokwenda kutumika katika nchi mbalimbali ikiwemo, Madagascar, Msumbiji, Malawi,Zambia, Congo DRC, Burundi, Uganda, Kenya na Rwanda. Pia wachungaji na watumishi wamekuwa wakitumika katika kuhubiri na kufundisha Neno la Mungu nchini kote.

Kuelekea kilele cha maadhimisho 85 ya kuanzishwa kwa kanisa hilo nchini kutakuwa na ibada kubwa ya kumshukuru Mungu pamoja na kuandaa shughuli kadhaa zinazolenga kuhamasisha jamii kuhimiza umoja na mshikamano ikiwa ni pamoja na semina maalumu ya uongozi kwa viongozi wa ngazi za juu wa Serikali na vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na kongamano kubwa la vijana ambapo vijana zaidi ya 10,000 wenye umri chini ya miaka 34 wataudhulia.

Aidha Dkt. Mtokambali ameishukuru Serikali katika awamu zote tangu kuanzishwa kwa kanisa hilo nchini kwa kuwapa ushirikiano mkubwa tangu enzi ya Hayati Mwalimu Nyerere hadi sasa awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan.