Breaking News

TANZANIA TOP REKODI (TTR) KUFANYA MATEMBEZI KUENZI MCHANGO WA WALIOJITOA KWA TAIFA

Katika kutambua na kuenzi mchango wa viongozi mbalimbali Taasisi ya Tanzania Top Record (TTR) imeandaa matembezi ya kilometa moja peku (bila viatu) ikiwa ni ishara ya kuenzi viongozi na watu mbalimbali ambao wamepambania taifa na kuacha alama hapa nchini.

Akizungumza jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi hiyo, bwana Rahimu Idd amesema pamoja na kuratibu matembezi hayo pia taasisi hiyo itashughulika na ukusanyaji, uchakataji wa taarifa za mbalimbali za makundi ya watu ikiwemo viongozi wa dini, wanasiasa, wanamichezo wengineo. 

Amesema lengo la kufanya kwa matembezi hayo ni kutambua watu ambao katika nyanja tofauti nchini wamefanya vitu vya kuwasaidia jamii na kuacha alama ambazo zinastahili kuigwa kizazi hadi kizazi ili kuleta mfanikio kwa taifa na kudumisha amani iliyopo.

“Tunaamini wapo viongozi na jamii nyingi ambao wamefanya makubwa nchini na inawezekana mchango wao usionekana kwa sababu mbalimbali ingawa ukikaa ukitulia unaona na kitu fulani kimefanywa na mtu na imesaidia kuleta maendelea nchini". Alisema na kuongeza kuwa

“Mfano Rostam Azizi yeye ndiye alitoa wazo kwa la bima ya afya kwa wananchi wake 
wakati alipokuwa Mbunge jambo ambalo rais wa wakati huo, Hayati Benjamin Mkapa alilibeba na kuwa la kitaifa, sasa hiyo ni alama ambayo Rostam ameiweka na inastahili kusemwa na kuhifadhiwa kama sehemu ya kumbukumbu nchini,”. Alisema Bw. Idd.

Aida Bw. Idd aliongeza kuwa ukiachana na Rostam wapo viongozi wengi ama watu wa kawaida wameweka alama na hawatajwi, hivyo taasisi itakuwa ni sehemu ya kuwaibua kuwaweka kwenye majarida na kuwatangaza ili jamii iwajue na waheshimike kizazi hadi kizazi.

Alisema taasisi hiyo imejipanga kutoa tuzo kwa watu mbalimbali kwa lengo la kutambua mchango wao nchini ili kusaidia kusukuma wengine ambao wapo kwenye nafasi kufanya vizuri zaidi kwa maendeleo ya nchi. 

Akizungumzia matembezi hayo ambayo yatatumia dakika 20, yatatoa fursa kwa viongozi wa dini pia kuliombea taifa ili lidumu kwenye amani, umoja na utulivu kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Oktoba mwaka huu na Rais, Wabunge na Madiwani mwakani.
 
“Sambamba na kufanya matembezi pia tutamwombea Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na tayali tumeshamwomba ikiwa ataridhia siku hiyo utupe ujumbe kwa ajili ya Watanzania hususan vijana wa kizazi hiki na vijavyo tuwe wamoja licha ya kuwepo changamoto za siasa na kiuchumi,”. Alisema Bw. Idd