Breaking News

WANANCHI TUSHIRIKIANE KUFICHUA WAHALIFU.


Na HADIA KHAMIS
Mkaguzi Msaidizi wa Jeshi la Polisi (A/INSP) Paschal Deus Kafula ambaye ni Polisi Kata wa Kata ya Makangarawe Wilaya Temeke amewataka wananchi kuendeleza mahusiano mazuri na jeshi la Polisi ili kutokomeza vitendo vya kihalifu.

Ushauri huo ameutoa Jijini Dar es Salaam wakati walipokuwa wakifanya mazoezi (joging) kwa kushirikiana na Polisi shirikishi na wananchi mbali mbali wa Kata hiyo.
Kafula amesema kuwa ili kutokomeza uhalifu ni lazima kuwepo na ushirikiano baina ya jeshi la Polisi na wananchi.

"Niwatoe hofu wananchi ya kwamba Polisi ni raia kama raia wengine ni vyema tushirikiane kwenye masuala mbali mbali kama hivi mazoezi lakini pia tusiache kuwafichua wahalifu kwa kufanya hivyo tutaweza kuidhibiti kwa asilimia 100 Kata yetu Na wahalifu," amesema kafula.

Amesema kuwa nyinyi wenyewe ni mashahidi wa tulipotoka na sasa tulipo kwa kiasi kikubwa tumefanikiwa kuidhibiti wahalifu hivyo hatutakiwi kuridhika na Hali ilivyo.

"Ikumbukwe kuwa kila siku muhalifu anatafuta mbinu mpya ya kufanya uhalifu lakini tukishirikiana tutaweza kudhibiti mbinu zote za wahalifu", Alisema kafula.