Breaking News

PROF. LIPUMBA YUPO NCHINI BURUNDI KUIWAKILISHA TCD

THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-Chama Cha Wananchi)

TAARIFA KWA UMMA:
Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (Tanzania Center for Democracy-TCD) na Mwenyekiti wa CUF - Chama Cha Wananchi Prof. Ibrahim Lipumba yupo safarini Burundi kuiwakilisha TCD kwenye Warsha Maalum kwa ajili ya kuchagiza vyama ambavyo havijaunga nguvu kwenye Jukwaa/Baraza la Vyama vya Siasa la nchi hiyo (Permanent Forum for Dialogue of Approved Political Parties in Burundi - FDP) kufanya hivyo. FDP ilianzishwa mwaka 2009.

Prof. Lipumba aliyesafiri Alhamisi Aprili 25 anatarajiwa kurejea nchini Jumamosi Aprili 27, 2024 baada ya kushiriki Warsha / Mkutano huo wa siku moja (26 / 04 / 2024).

HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE!

Eng. Mohamed Ngulangwa
Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma
CUF- Chama Cha Wananchi
Aprili 25, 2024