Breaking News

ASKARI WAWILI WAJERUHIWA AJALI YA MOTO MLANDIZI

Na Mwandishi Wetu, Pwani 
ASKARI wawili wa Jeshi la Zimamoto na uokoaji wamejeruhiwa wakiwa katika harakati za kuokoa marehemu waliokuwa wamenasia kwenye gari baada ya kuzuka moto ghafla na magari kuwaka moto .

Hayo yamesemwa leo Machi 28 na Kamanda wa Polisi Mkoa Mkoa wa Pwani (SACP) Pius Lutumo alipozungumza na Waandishiwa
Habari .

RPC Lutumo amewataja askari waliojeruhiwa kuwa ni Koplo Elias Bwire na Koplo Hamisi Kungwi wote wamekimbizwa Hospitali ya Taifa Mloganzila kwa matibabu na hali zao zinzendelea vizuri. 
" Machi 28 mwaka huu majira ya saa 10:15 alfajiri katika bonde la Ruvu Wilaya ya Kipolisi Mlandizi, Mkoa wa Pwani barabara ya Morogoro, Dar es Salaam gari namba T668 DTF aina ya Scania Kampuni ya Sauli ikiendeshwa na dereva Idd Aloyce (35),mkazi wa Mafinga ikitokea Dar es Salaam kwenda Mbeya liligonga ubavuni lori la mafuta ya Petroli lenye namba za usajiri RAF672N na tela lenye namban RL2594 aina ya Howo lililokuwa linatoka Dar es Salaam kwenda nchini Rwanda likiendeshwa na dereva Mushimana Musiyimana lililokuwa limesimama kupisha gari lililokuwa linakuja mbele yake".

Aidha basi hilo lilikuwa limeongozana na basi la Golden Deer Kampuni ya New Force lenye namba za usajiri RAF672N na likiendeshwa na dereva aitwaye Burton Jacob (33),.mkazi wa Mbeya ambapo nalo lililigonga kwa nyuma basi la Saul lililokuwa mbele yake na kusababisha vifo vya watu wawili ambao hawakufahamika majina yao na majeruhi watatu ambao ni Salimu Daud (50) mkazi wa Mbozi Mbeya, Farida Idrisa (26)mkazi wa Tabata Dar es Salaam na Kiambile Geofrey mkazi wa Uyole Mbeya. 
RPC Lutumo chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa madereva wa mabasi yote mawili kushindwa kuchukua tahadhari kwa kuyapita magari mengine lakini pia kushindwa kutunza umbali kati ya gari moja na lingine huku yakiwa yamefatana.

"Pamoja na hayo uchunguzi wa awali unaonesha kuwa chanzo cha moto huo ni hitilafu ya injini ya basi la Saul iliyokua imekita chini baada ya kugonga gari lingine na kuripua petroli wakati wa uokoaji"amesema RPC Lutumo.
"Wito wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani unawataka madereva kutii sheria za Usalama Barabarani kwa mujibu wa taaluma zao na ifahamike kwamba madereva wanachukua dhamana kubwa ya maisha na mali za watu"

Mkuu wa mkoa wa Pwani Abubakari Kunenge amesema atayafungia mabasi yatakayoendelea kuvunja Sheria za Usalama Barabarani baada ya ajali iliyotokea alfajiri ya leo.

RC Kunenge amesema hayo wakati akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisini kwake Kibaha Mkoani Pwani, amesema yeye ameamua kwa kushirikiana na wanaotoa lesseni, LATRA na Jeshi la Polisi kuwa wataweka mkakati wa kudhibiti ajali ndani ya Mkoa wa Pwani.

"Mtagundua kuwa Mkoa wa Pwani hii Barabara ni kubwa na mabasi yakitoka kule stendi kuu ya Dar es salaam Mbezi idadi ya mabasi ni mengi yakiwa yamekaguliwa lakini bado hapa pia tunakagua " amesema.