Breaking News

RAIS DKT. SAMIA ATAJWA UJIO WA NDEGE YA SAUDIA AIRLINE, WATANZANIA KUNUFAIKA.

IMEELEZWA kuwa ushiriki wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania,Samia Suluhu Hassan katika kushiki kwenye Filamu ya Royal tour kumechangia katika kuinua sekta ya Utalii nchini na kuwavutia wawekezaji mbalimbali kuja katika kuwekeza kwenye usafiri Anga.

Hayo yameelezwa leo Jijini Dar es Salaam na  Meneja Mauzo wa ndege ya Saudia  airline,Rehana Mukadam ,wakati akizungumza na Waandishi wa habari katika maonesho makubwa ya utalii yanayoendelea katika ukumbi wa mlimani city jijini Dar es Salaam.

"Ukiangalia sahivi Tanzania imekuwa na ukuaji mkubwa wa utalii,ukifuatilia mwenyewe Rais ameweza kutuandalia filamu inayoonesha uzuri na ufahali wa nchi yetu na hii tunasema mchango wake umechangia ujio wa ndege hii ya Saudia Airline"Amesema Rehana.

Aidha,Rehana,amezungumzia ujio wa ndege ya Saudia airline amesema teyari imeshaanza kutoa huduma nchini itakuwa inaruka mara ya nne kwa wiki kwa bei nafuu na kuchangia kuifungua Tanzania kibiashara kutokana na wasaudia kuingia nchini na Watanzania kwenda Saudia.

Hata hivyo,Rehana amesema ujio wa ndege hiyo pia umewarahisisha kwa mahujaji wa kislam wanaokwenda kusali nchini humo.

"Hii ni fursa kubwa kwa wafanyabiashara kutumia ndege hii kwa ajili ya kwenda kufanya biashara saudia,"amesema 

Kadhalika,Rehana amesema Ndege za saudia zinakwenda sehemu mbalimbali duniani kwa bei nafuu huku akisema wameanza kutoa viza kwa kila mtu anayetaka na kuwataka watanzania kuchangamkia fursa hiyo.

"Hii ni fursa kwa Watanzania tunavyokuwa tunakwenda nchini kwao na wao wakija nchini itasaidia kuleta fursa kwa biashara."

Kwa upande wake Balozi wa Saudia nchini,amesema uhusiano wa Tanzania utasaidia kuchangia katika kukuza sekta ya utalii katika utalii katika mataifa hayo.

No comments