HAMADI RASHID: HAKUNA MUNGU MTU NDANI YA ADC
Chama cha Alliance for Democratic Change (ADC) kimesema hakuna Mungu Mtu katika chama hicho ambapo wakati ukifika viongozi wenye dhamana kubwa akiwemo Mwenyekiti huachia ngazi ili kupisha wengine.
Mwenyekiti wa ADC Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed aliyasema hayo katika mahojiano maalumu na mwandishi wa mtandao huu makao makuu ya chama hicho Buguruni mkoani Dar es Salaam hivi karibuni.
Alisema chama hicho kimejiwekea utaratibu mzuri wa uongozi ikiwepo kufanya uchaguzi wa kuwapata viongozi mbambali katika nafasi zote za uongozi ikiwemo nafasi ya Mwenyekiti Taifa wa chama hicho na kusema kwamba mKutano mkuu utaanza April 2024 na kutamatika Mei 2024 na utatatua kitendawili cha nani atakuwa Mwenyekiti Taifa.
“Kila wakati narejelea misingi ya ADC ambayo imejengeka katika misingi imara ya utu, uchaji wa Mungu na demokrasia ya haki. Ni chama ambacho kinalenga kuwajenga viongozi waadilifu kwa manufaa ya taifa kwa vizazi vyote hivyo Kanuni na Katiba yetu kiongozi huhudumu miaka 5 ya awali na kisha huruhusiwa kugombea awamu ya pili endapo hana pingamizi lolote na mimi nimehudumu kwa miaka yangu kumi kikamilifu lakini tunasubiri uchaguzi mwakani utatoa jibu nani atafaa kiti cha uongozi wa kitaifa” alisema Hamad Rashid
Chama hicho ambacho kilianzishwa 2012 kimetimiza miaka 10 mwaka jana kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika ndani ya ADC uchaguzi wa Mkutano Mkuu utafanyika mwakani kama ilivyoelezwa hapo juu.
Akizungumzia utofauti wa vyama vingine nchini, ADC kinatambua na kuheshimu uwepo wa Mwenyezi Mungu. Hiyo ni moja ya misingi mikuu ya uongozi ndani ya ADC.
“ADC inaamini kiongozi mwenye kumcha Mungu atakuwa mwadilifu na mwenye kutenda haki kwa wananchi wananchi na ndiyo maana sisi tunachukia rushwa na hatuna kashifa za rushwa ama ubadhirifu ndiyo maana husikii migogoro isiyokuwa ya maana ndani ya ADC” alisema Mhe. Mohamed
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Fedha Taifa na Katibu wa Bodi ya Wadhamini ya ADC bwana Hassan Mvungi alisema chama sasa kinawekeza zaidi katika uchumi wa kidijiti ambapo wanachama hufundishwa namana ya kutafuta fursa za kujikwamua kiuchumi na kuwasaidia wananchama wao ili wasidhalilike kwakujihusisha na vitendo vya rushwa.
“Kwakuwa hatuna maluplupu na ruzuku tumewafundisha wanachama wetu kujitegemea kiuchumi zaidi ambapo tuna vikundi vya wezesha vikoba dhidi ya wanachama wetu na vikundi hivyo vingi vimejimarisha kiuchumi kiasi cha kufikisha hadi mtaji wa milioni 40 kwa kikundi kimoja haya ni mafanikio makubwa ambapo wengine hawana budi kuiga mfano huu kwa ADC “alisema Mvungi
Akizungumzia kuimarika demokrasia katika chama hicho alisema hata jina lenyewe linasadifu kwamba ni waumini wakubwa wa demokrasia nchini ndiyo maana hawana tabia ya kususia uchaguzi wote na kusema kwamba hata uchaguzi wa hivi karibuni uliohusisha mgombea ubunge wa Mbarali mkoani Mbeya walishiriki na walishiriki kinyanganyiro cha udiwani katika majimbo mbalimbali katika uchaguzi huo.
Kuelekea uchaguzi Mkuu, Mvungi alisema watakiwasha vilivyo katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani kisha kushiriki vilivyo katika uchagzuzi mkuu wa 2025 nakuwatumia salamu wapinzani wao kuijpanga zaidi kwani ADC ni chama kikubwa na siyo kichanga kama baadhi ya watu wanavyokinadi.
No comments