MAVUNDE AONGOZA MJADALA WA MCHANGO WA SEKTA YA FEDHA KWENYE MADINI
Dar es Salaam
Waziri wa Madini Mhe. Anthony Mavunde leo Oktoba 5, 2023, anaongoza majadiliano maalumu kuhusu mchango wa sekta ya fedha katika ukuaji wa sekta ya madini .
Kikao hicho kinachofanyika katika Hoteli ya Serena Jijini Dar es Salaam kinahudhuriwa na Taasisi kumi za Umma na binafsi zinazojishughulisha na sekta ya fedha chini ya mwamvuli wa Umoja Wa Mabenki Tanzania ( TBA).
Wengine wanaohudhuria mkutano huo muhimu kwa msatakabali wa maendeleo ya sekta ya madini nchini ni pamoja na wafanyabiashara wa madini, watoa huduma, wachimbaji wadogo, wa kati na wakubwa.
Taasisi za fedha kwenye mkutano huo ni pamoja na CRDB, NMB, NBC, BOA pamoja na benki ya Amana
No comments