Breaking News

NAIBU WAZIRI UTALII KITANDULA KUONGOZA UTALII WA NDANI KUTEMBELEA HIFADHI YA KAZI MZUMBWI KILELE CHA NYERERE DAY

Mratibu na Msemaji wa Shirika  lisilo la kiserikal la Community Distinguished and Envirometal Conservation, (CODECO) bwana Steven Nchimbi akizungumza katika mkutano na waamdishi wa habari( hawapo pichani) juu ya maandalizi ya kutembelea hifadhi ya Kazi Mzumbwi iliyopo Kijiji cha Kazi mzumbwi wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani
Ofisa Utalii wa TFS wilaya ya Kinondoni, Bi Catherine Melchory akifafanua juu ya ushiriki wao kuelekea kutembelea hifadhi ya Kazi Mzumbwi iliyopo Kijiji cha Kazi mzumbwi wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani

Dar es salaam:
Naibu Waziri wa Malia Asili na Utalii, Dunstan Kitandula anatarajiwa kuongoza kundi la watalii wa ndani na wakigeni siku ya kumbukizi ya mwalimu nyerere katika hifadhi ya Kazi Mzumbwi iliyopo Kijiji cha Kazi mzumbwi wilayani Kisarawe mkoa wa Pwani.

Hayo yalelezwa jana na Mratibu na Msemaji wa Shirika  lisilo la kiserikal la Community Distinguished and Envirometal Conservation, (CODECO) bwana Steven Nchimbi wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelekea kilele cha kumbukizi ya Muasisi wa Taifa na aliyekuwa Rais wa kwanza wa iliyokuwa Tanganyika (Tanzania) Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

‘’Shirika letu la Codeco kwakushirikiana na Wakala wa Misitu Tanzania (TFS) na Kampuni ya utengenezaji na uuzaji samani nchini (Mfugale Funiture) tumeamua kuja na mpango huu ili kuenzi kazi nzuri zilizofanywa na Mwalimu Nyerere enzi za uhai wake ikiwemo shughuli za uhifadhi’’ alisema Nchimbi

Alisema Shirika hilo kwa kushiruikiana na TFS wataendelea kutoa elimu kwa jamii na haswa kizazi cha sasa ambapo watoto wengi hawafahamnu mambo mbalimbali nan yeti yaliyofanywa na Mwalimu wakati wa uhai wake.

‘’Sanjari na utoaji elimu ya uhifadhi wa mazingira ikiwemo kuzalisha miche ya miti tunampango wakutoa elimu ya mazingira na kazi za Mwalimu Nyerere kwa mapana zaidi ikiwemo kuandaa midahalo katika vyombo vya habari kuendelea kuunga mkono yote yaliyofanywa na Mwalimu lakini zaidi kufundisha uzalendo kwa watoto wetu na uzalendeo wenyewe ni pamoja na utunzaji wa mazingira’’ alisema bw. Nchimbi

Kwa upande wake Ofisa Utalii wa TFS wilaya ya Kinondoni, Catherine Melchory alisema wamechagua Kazi Mzumbwi badala ya eneo lingine kwakuwa ni karibu na wilaya nyingi za mkoa wa Pwani na kwa wakazi wa Dar es Salaam.

‘’Kazi mzumbwi ipo jirani na Dar es Salaam na wilaya za mkoa wa Pwani hivyo tunawakaribisha wakazi wote wa mikoa ya jirani na mkoa wa Pwani, wageni kutoka mataifa mbalimbali tuje tuazimishe siku hii adhimu kwa Baba wa Taifa letu’’ alisema

Naye Ofisa Uhusiano wa Mfugale Funicher, Bi. Neema Lymo alisema wafanyabiashara wa mazao ya misitu na wadau wa mazao ya misitu siyo watu wakukosa tukio hilo.

‘’Ni muhimu kwa wadau wa misitu kuhudhuria tukio hili wajionee vivutio mbalimbali vilivyopo Kazimzumbwi, magari yatakuwepo siku ya safari pale Mlimani City, Mbezi Lous, Mpingo House na Ubungo Oilcom kuanzia saa 12;00 asubuhi Septemba 14

Kadhalika kutakuwepo na burudani mbalimbali, vinywaji,ngoma za asili, disko kwa Sh 3,5000 tu kwa mtu mmoja unajipatia tiketi ya ushiriki wako itakayohusisha yote yaliyoorodheshwa tiketi zinapatikana Mpingo house ofisi za TFS, Mwenge Vinyagio chumba Namba 15.

Oktoba 14 kila mwaka Tanzania huadhimisha siku ya kumbukizi ya kifo cha Mwalimu Nyerere ambapo mwaka huu atatimiza miaka 24 tokea atwaliwe na Muumba wa Mbingu na nchi. 

No comments