Breaking News

ATLAS SCHOOLS HALF MARATHON 2023 KUUNGA MKONO JITIHADA ZA SERIKALI KUTOKOMEZA UKATILI

Mwalimu Willbroad Prosper kutoka Shule za Atlas akifafanua jambo katika mkutano na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akitangaza zawadi za washindi wa mbio za Kilomita 5 kwa watoto, kilomita 10 na 21 kwa watu wazima
Mwalimu Willbroad Prosper kutoka Shule za Atlas akiwaonyesha waandishi wa habari moja ya Fulana zitakazo tumika kesho katika mbio Atlas Schools Half Marathon 2023 jijini Dar es salaam.
Mwalimu Prosper akionesha medali za washindi watakaoshiriki mbio za Atlas Schools Half Marathon 2023 Kesho Oktoba 14, 2023 jijini Dar es Salaam.
Mwalimu Willbroad Prosper kutoka Shule za Atlas akionesha baadhi ya namba zitakazo tumika kesho kwenye Mbio za Shule za Atlas Schools Half Marathon 2023 jijini Dar es Salaam. Picha zote na Avila Kiango 

Dar es salaam
Tanzania ikiwa inaadhimisha miaka 24 ya kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Nyerere ambayo uadhimishwa kila 14 oktoba shule ya Atlas imendaa mbio za Atlas Schools Half Marathon 2023 kwa lengo la kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwalinda watoto na jamii dhidi ya ukatili.

Akizungumza juu ya maandlizi ya mbio hizo jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya Atlas Schools Half Marathon 2023, Mwalimu Wilbroad Prosper amesema kwa mwaka huu mashindano hayo yameboreshwa zaidi na kuwa na ushawishi na msisimko kubwa ambapo washiriki wataweza kukimbia umbali wa kilomita 5, 10 na 21.

“Mwaka huu tumeganya maboresho makubwa kwa kushirikiana na  Mamlaka za usajili wa Riadha Tanzania (RT), Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam (DAA) pamoja na Baraza la Michezo la Taifa (BMT) hivyo kuwa na msisimko na ushawishi mkubwa ikilinganisha na mwaka uliopita" Alisema Mwalimu Prosper.

Alisema kufatia maboresho hayo mwaka huu, kumekuwepo na mwitiko na ushawishi kwa watu wengi hivyo wamejiandaa vyema kuhakikisha washiriki wote wanapata huduma muhimu kama vile fulana, namba (Bibs), begi la kimichezo (Kitbag), Wristband, Matunda, Vinywaji njiani, Nyama choma, burudani na Medali baada ya kukimbia.

Amesema katika mbio za mwaka huu zitawakutanisha washiriki mbalimbali ikiwemo watu binafsi, makampuni, taasisi za serikali na binafsi, wanafunzi, makundi mbalimbali ya wakimbiaji pamoja na wadau wa michezo huo ambapo kila mshiriki atachangia shilingi 35,000 tu.

Mwalimu Prosper aliongeza kuwa katika kuhakikisha mashindano ya mwaka huu yanakuwa ya kipekee wametoa nafasi kwa vikundi kushirikk ambapo kwa wale wanaojisajili katika makundi watalipia shilingi 32,000.

"Kamati ya maandalizi ya Atlas School s Half Marathon mwaka huu imejipanga vizuri kwa kuboresha na kuandaa mazingira mazuri hususani njia zote zitakazotumiwa kupimwa na kukaguliwa na wataalamu kutoka Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam zimepitiwa na kuonekana zina ubora unaohitajika" Alisema Mwalimu Prosper.

Amezitaja njia zitakazotumika kwa wakimbiaji wa 5 km wataanzia Shule ya Atlas Madale, kuelekea Six Pub mpaka Joy Eslava na kurudi mpaka shuleni kupitia geti la nyuma na kurudi sehemu ya kuanzia mbio (Finishing Point), wakimbiaji wa 10 km wataanzia shuleni kuelekea Six Pub mpaka njia Nne karibu na SAI SAI na kurudi shuleni kupitia geti la nyuma mpaka mpaka eneo la kumalizia mbio (Finishing Point).

Ametaja nyingine kuwa wakimbiaji wa 21 km wao wataanzia shuleni kuelekea njia ya Tegeta lami, mpaka Flamingo na kuendelea mpaka Montana Bar ambapo itageuzia hapo na kurudi mpaka Six Pub, kuelekea njia Nne mpaka SAI SAI na kugeuza kurudi kupitia geti la nyuma mpaka kwenye eneo la kumalizia mbio (Finishing Point).

Kwa upande wake Katibu wa Chama cha Riadha Mkoa wa Dar es Salaam, bwana Samwel Mwera ameshukuru kwa namna Shule za Atlas zinavyoandaa mbio hizo kwani wamekuwa wakishirikiana hatua kwa hatua na kwamba uongozi wa shule umekuwa ukifuata taratibu zote.

Naye Mjumbe wa Kamati ya Ufundi kutoka Mamla za Usajili Riadha Ranzania (RT) Kanda ya Pwani, bwana Felix Chunga amesema Shule za Atlas zimekuwa ni mdau wao mkubwa na wamekuwa wakishirikiana kwa msimu wa tano sasa.

Amesema ni wajibu wao kuhakikisha wanasimamia mbio hizo kwa kufuata taratibu na sheria, hivyo wamekuwa wakishirikiana na Shule za Atlas kuboresha mbio hizo.

Mbio za mwaka huu zimebeba kaulimbiu isemayo “Tokomeza ukatili dhidi ya Watoto” ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwalinda Watoto na jamii dhidi ya ukatili.

No comments