JUMUIA YA MARIDHIANO NA AMANI TANZANIA (JMAT) YANADI MAFANIKIO YA ZIARA ZAKE KIMATAIFA
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania, Sheikh Dokta Alhad Mussa Salum akifafanua jambo wakati akizumgumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu ya mafanikio ya ziara za kimataifa makao makuu ya (JMAT) jijini Dar es salaam.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania Askofu Dokta Israel Ole-Gabriel akiongea katika mkutano huo na waandishi wa habari juu ya faida za ziara za kimataifa nchini Iran, Korea kusini na Kenya makao makuu ya (JMAT) jijini Dar es salaam.
Dar es salaam
Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) imetangaza mafanikio ya ziara za kimataifa zilizofanywa na Vongzozi wa jumuia hiyo wakiongozwa na mwenyekiti wake Dokta Alhad Mussa Salum katika mataifa mbalimbali duniani.
Akizungumza Jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa (JMAT), Askofu Dkt Israel Ole-Gabriel Maasa amesema ziara hizo zimefanyika kufatia kupata mwaliko wa kuhudhuria Mkutano wa Amani wa Kimataifa, uliowakutanisha Viongozi wa Dini na Wadau Mbalimbali wa Amani duniani.
Amesema mkutano huo ambao ulifanyika kuanzia 17 hadi 19 mwezi Agosti nchini korea kusini katika jiji la Seoul mwenyekiti wa JMAT aliambatana na viongozi wa ngazi mbalimbali.
"Mkutano huu uliondaliwa na shirika la Kimataifa la Amani lijulikanalo kama Heavenly Culture World Peace Restoration of Light (HWPL). Mwenyekiti aliambatana na viongozi wawili wa Kitaifa ambao ni Mratibu JMAT Bi Fatma Fredric Kikkides na Mkurugenzi wa Idara ya Kuu ya Mipango, Fedha, Uchumi na Utekelezaji". Alisema Askofu Dkt. Israel.
Alisema kupitia mkutano huo JMAT imepata faida kubwa ikiwemo Kusaini Mkataba wa kufanya kazi pamoja na Shirika la HWPL juu ya masuala ya Amani Duniani, kujenga Mahusiano ya Kimataifa na Taasisi za Kimataifa pamoja na kukuza mtandao kwa kufanyakazi na watu wengi kwaajili ya Amani Duniani.
"Kupitia mkutano huo Mratibu JMAT Taifa, Bi. Fatma Fredric Kikkides alichaguliwa kuwa Ubalozi wa Amani Duniani kupitia Shirika tanzu la HWPL linaloshughulikia Amani Duniani kwa wanawake liitwalo International Women Peace Group (IWPG)" Alisema Askofu Dkt. Israel.
Alisema 26 September mwaka huu viongozi wa JMAT pia walipata mwaliko wa kwenda Nchini Kenya jijini Mombasa kuwa mgeni rasmi katika shughuli ya kumtawaza Mufti Mpya wa Kenya Sheikh Mshali Khamis Mshali Ashiraazy kupitia taasisi ya Kemnack Nchini Kenya.
Askofu Dkt. Maasa aliongeza kuwa 30 Septemba mwaka huu viongozi wa JMAT Taifa alipata mwaliko wa kuhudhulia mkutano wa Umoja wa Umma wa kiislam na Mahusiano ya Dini mbalimbali jijini Tehran Nchini Iran, Mkutano uliofunguliwa na Rais wa Iran Mheshimiwa Ayatollah Sayyid Ibrahim JMAT.
"Katika Mkutano huu Mwenyekiti wa JMAT Taifa alipata nafasi ya kutoa Hotuba juu ya masuala ya Umoja wa Kiislamu, Mahusiano ya Dini mbalimbali ulimwenguni pamoja na Masuala mbalimbali yanayohusu Amani Duniani". Alisema Askofu Dkt. Israel.
Nae Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) Sheikh Dokta Alhad Mussa Salum amesema kupita ziara hiyo amejifunza Mambo Mengi ikiwa ni pamoja na Umuhimu wa kulinda Amani kwani Mataifa kama Korea Kusini na Iran yamekuwa mstali wa mbele kuisistiza jamii kuendelea kushirikiana kudumisha Amani kutokana athari walizozipata kutokana na vita
"Wenzetu wa Iran na Korea Kusini tayali wameshaona athari za kutokuwa na amani na hawataki tena kuingia huko, wakati sisi Tanzania Wakristo na Waislam tunavumiliana, tunakaa pamoja, tuendelee kudumisha Amani ya Taifa letu kwani ndio Tunu yetu". Alisema Sheikh Dkt. Mussa.
Kwa upande wake Mratibu wa JMAT Taifa na balozi wa Amani Duniani, Bi. Fatma Kikkides amesema kupitia ziara hiyo amejifunza mengi na sasa anaendelea na mafunzo maalumu juu ya amani.
"Nimejifunza Mambo Mengi Sana hususani kuhusu vita na Machafuko kwani waanga wakubwa ni Wanawake na Watoto hivyo nina jukumu la kulinda watoto na familia nzima kimwili na kiakili, nitakapo hitimu mafunzo nitaendelea kutoa elimu kwa jamii juu ya kudumisha Amani Tuliyonayo" Alisema Bi. Fatma
No comments