Breaking News

UWT INATAMBUA MCHANGO WA ASASI ZA KIRAIA KATIKA KUWASAIDIA WANAWAKE NA WATOTO

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Bi Mwajabu Mbwambo amesema UWT inatambua mchango wa asasi zisizo za kiserikali hususani zenye mpango wakusaidia wanawake, mabainti na watoto.

Bi Mwajabu aliyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari juzi baada ya mafunzo kwa wanawake wa jasiriamali yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji Tanzania (NIT)

”Niwaunge mkono na kuwapongeza  Taasisi ya Voice of Eagle kutokana na mchango wao wa dhati wakuwainua wakina mama na mabinti kwakuwapatia mafunzo ya biashara kwakufanya hivyo wanaungana nasi katika utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ya 2020-2025 hivyo tunatambua mchango wao na tunauthamini sana waendelee vivyo hiyo” alisema

Mwajabu ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mafunzo hayo aliwataka wakina mama pamoja na majukumu waliyonayonayo wasisahau malezi bora kwa watoto kwakuwa watoto hutegemea malezi bora kutoka kwa wazazi pamoja na changamoto mbalimbali.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo, meshack Robert mafyeko alisema hadi sasa wanawake wapatao 198 wamesaidiwa kupitia mafunzo ya ujasiriamali wakiwemo mamalishe, wafanyabiashara wadogo na mabinti kwakuwapa mafunzo ya ufundi stadi.

”Lengo la Taasisi nikuhakikisha mwanamke anapatiwa mafunzo kwa lengo la kumkomboa kiuchumi zaidi, maana wanaweza kuwa na mitaji lakini wasijue namna ya kuendesha biashara zaidi nakujikuta hawasongi mbele na badala yake huishia kulipa madeni ama marejesho kwa taasisi walizokopa” alisema mafyeko

Alisema miongoni mwa wanufaika wa mafunzo hayo nakueleza kwamba mafunzo hayo yamekuja wakati muafaka kwakuwa wengi wao hawana uwelewa wa biashara hivyo yatawasaidia katika shughuli zao za kila siku.

Joanitha Jeremia ni miongoni mwa wanufaika alisema” Ninashukuru kupata fursa hii kupitia Kampeni iitwayo ’binti mwenye ndoto’ imeniwezesha kupata mafunzo ya usanifu kurasa nchini Kenya hususani ubunifu na uaandaji wa taarifa za masoko kidijitali na sasa nimeanza vyema kazi hiyo ambapo natafuta wateja” alisema

Vilevile Joanitha alisema kwamba amehitimu Stashahada ya ufamasia lakini bado haja bahatika kupata ajira serikalini wala sekta binafsi na alipoipata fursa hiyo aliichangamkia  jambo ambalo akipata mtaji atafanya vyote kwa pamoja yaani ufamasia na usanifu kurasa kwakuwa teknolojia imekuwa haoni shida kutimiza majukumu hayo kwa pamoja.

Katika mafunzo hayo taasisi mbalimbali zilitoa mada mbalimbali za biashara wakiwemo  Mfuko wa kujikimu wa UTT, AMIS na Shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo (Sido) pamoja na Shirika la  Viwango Tanzania (TBS)






No comments