CUF WATOA TAMKO SAKATA LA UHABA WA MAFUTA, WAITAKA SERIKALI KUCHUKUA HATUA ZA HARAKA
THE CIVIC UNITED FRONT (CUF-Chama Cha Wananchi)
UHABA WA MAFUTA WASABABISHA TAHARUKI, SERIKALI ICHUKUE HATUA HARAKA:
CUF-Chama Cha Wananchi kimebaini juu ya uwepo wa uhaba wa mafuta maeneo mbalimbali nchini, hali inayosababisha taharuki.
Hali mbaya zaidi imedhihirika mkoani Tabora ambapo magari na bodaboda zinapanga foleni muda mrefu kwenye vituo vya nishati hiyo na kupelekea shughuli nyingi kukwama. Aidha kutokana na upungufu huo, baadhi ya vituo vya mafuta vimeweka viwango vya juu vya mafuta ambapo bodaboda inauziwa si zaidi ya lita mbili na magari si zaidi ya lita sita (6) huko Tabora.
CUF- Chama Cha Wananchi kinatoa wito kwa Serikali kuvunja ukimya na kuzungumzia hali hii na, muhimu zaidi, kuchukua hatua za haraka kutatua tatizo hili kabla ya athari kubwa zaidi kutokea.
HAKI SAWA NA FURAHA KWA WOTE!
Eng. Mohamed Ngulangwa
Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma
CUF- Chama Cha Wananchi
Septemba 5, 2023
No comments