NAIBU WAZIRI MKUU DKT. BITEKO AFUNGA KONGAMANO LA AGRF
Naibu Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko akihutubia wakati akifunga mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika kwa mwaka 2023 (AGRF 2023) katika ukumbi wa kimataifa wa mwalimu Julias Nyerere (JNCC) Jijini Dae es salaam.
Dar es salaam;
Naibu Waziri Mkuu Mhe. Dkt. Doto Biteko kwa niaba ya Waziri Mkuu amefunga Rasmi Kongamano la mifumo ya Chakula lililofanyika JNICC.
Akifunga Kongamano hilo Mhe. Dkt. Naibu Waziri Biteko amesema “Kongamano hili limetaka kuwepo kwa uongozi thabiti ili kuleta mabadiliko yatakayoleta uwekezaji na limetoa jukwaa kwa viongozi na watengeneza sera likilenga vijana na wanawake kuweza kutumia vizuri rasilimali zilizopo.”
Aidha amezitaka Serikali za Afrika kuweka uwiano katika sera zao ili kuwepo kwa mabadiliko katika Sera za Chakula.
Mwisho amemaliza kwa kuwakaribisha tena kufanyia Kongamano lingine Dar es Salaam huku akiamini jukwaa lingine mwakani litakuwa na nguvu na washiriki wengi zaidi.
No comments