VANILLA INTERNATIONAL LIMITED YAWEKEZA KENYA
Kampuni ya Vanilla International Limited, yafungua mradi wa Vanilla Village Kenya, eneo la Mombasa mji mdogo wa Mariaani, baada ya kupokea maombi mengi kutoka nchini humo.
Mradi huo umefunguliwa na Mkurugenzi wa Vanilla International Limited, Simon Mnkondya, ambapo aliwapongeza wananchi wa Kenya kwa kutambua utajiri uliojificha katika uwekezaji huo, hivyo kutaka kuwekeza.
Mnkondya alisema amefanya uamuzi huo, baada ya Wakenya wengi kuonyesha uhitaji mkubwa wakuwekeza katika kilimo cha Vanilla, na kuvutiwa na mradi wa Tanzania, ambao unamashamba katika mikoa ya ARUSHA,ZANZIBAR na VANILLA VILLAGE DODOMA.
Mnkondya amewataka wakenya, kujitokeza zaidi kuwekeza katika kilimo cha Vanilla kwa mfumo wa mashamba Shufwaa yaani block Farming, kupunguza gharama za uwekezaji, kwa ajili ya usalama na kwa ajili ya kuhakikisha Uwepo wa soko la Vanilla.
Mr. Dipan Shah Mkurugenzi wa NYALI CINEMAX amesema VANILLA INDIA imewafanya wakulima wawe matajiri sana kwa maana ni zao la pili kwa bei duniani.
Mr.Bruno Cern'o Raisi wa Upendo Foundation mwenye Asili ya Italia amesema Kwa vile vanilla ni zao la bei kubwa ni vyema sasa Waafrika kulima Vanilla ili kupata utajiri endelevu na kuwa na unafuu wa maisha.
Lengo la mradi wa Vanilla Village Kenya ni kukuza uchumi wa wananchi hao na Waafrika kwa ujumla kwa sababu bei ya vanilla, imewahi kufikia Dola za Kimarekani 500$ takribani 1,000,000/= ya kitanzania ambapo wananchi wanaweza kuwasiliana na kampuni hiyo kwa namba ya +255629300200. Kenya +254 759604040
Post Comment
No comments