Breaking News

PROF LIPUMBA:APIGILIA MSUMARI WA MOTO KWA VYAMA VYA SIASA UIMARISHWAJI WA DEMOKRASIA NCHINI

Dar es Salaam;
Kituo cha Demokrasia Tanzania TCD kimezitaka Balozi zote nchini kuzidi kushirikiana nao katika kuendeleza Ujenzi wa Demokrasia ya Vyama vingi vya siasa kwani itazidisha haki, Amani maelewano na Ujenzi wa Uchumi Imara .

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), Mhe. Profesa Ibrahim Lipumba leo tarehe 22 Agosti 2023 katika Mkutano wa kitaifa kujadili hali ya Demokrasia nchini kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, vijiji na Vitongoji 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 uliofanyika Jijini Dar es salaam .

”Natoa wito kwa balozi zote zilizopo nchini, kushirikiana na Kituo cha Demokrasia Tanzania kuendeleza ujenzi wa demokrasia ya vyama vingi itakayodumisha haki, Amani, maelewano na ujenzi wa uchumi shirikishi utakaotokomeza umasikini .” Alisema Prof. Lipumba .

Hata hivyo naye Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa nchini, Bw. Sisty Nyahoza amezidi kusisitiza kuwa miongoni mwa kazi za Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ni pamoja na Kuvisajili na Kuvilea kwa lengo la kuleta Ushindani wa Siasa na Uchumi Imara kwa Wananchi.

”Jukumu la Ofisi ya Msajili ni kusajili vyama vya siasa na baada ya kuvisajili, ni kuvilea kwa kuhakikisha vinafuata sheria, na hata kuongeza Ushindani kwani ni muhimu katika kuleta maendeleo ya nchi yetu, lakini haya maendeleo ili yaje ni lazima tuendelee kukaa kwa amani, utulivu na umoja wetu tulio nao. ” Alisema Bw. Nyahoza


No comments