Breaking News

RC CHALAMILA: RAIS SAMIA ANATAKA MWANAWAKE ASIMAME KIUCHUMI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo leo wakati wa Semina ya mtaji wezeshi kwa wanawake na Vijana kwa hisani ya CRDB iliyokuwa inafanyika katika Ukumbi wa Tanzanite Kimara Wilaya ya Ubungo.

RC Chalamila amesema Rais Samia anataka mwanamke asimame kiuchumi ndio maana anaweka mazingira wezeshi kwa Taasisi za fedha kutoa mikopo yenye mashariti nafuu kwa wanawake hivyo acheni majungu changamkia fursa za kukua kiuchumi.

Hata hivyo RC Chalamila amesema ni ukweli usio pingika mwanamke akisimama kiuchumi Watoto watapata malezi bora na sio mwanaume. "mimi pia mkuu wenu wa mkoa napenda kuona mwanamke amesimama kiuchumi" alisema RC Chalamila

Aidha RC Chalamila ameahidi Kukutana tena na wanawake hao kutoa mchango wake, vilevile mafunzo hayo licha ya kufanyika kwa hisani ya CRDB yameratibiwa na madiwani wanawake wa viti maalum wa kata ya Saranga Kimara - Wilaya ya Ubungo

Ifahamike kuwa Benki ya CRDB imekuja na programu hiyo lengo kukuza, kuboresha na kumpa mtaji bila riba mwanamke anayetamani kujikwamua kiuchumi


No comments