Breaking News

DKT.JAFO AWATAKA WANANCHI KUSHIRIKI MAADHIMISHO YA WIKI YA MAZINGIRA KWA KUPANDA MITI.

Dodoma
Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mh. Dkt. Selemani Jafo amewataka watanzania kuungana kwa pamoja kushiriki maadhimisho ya wiki ya mazingira Kwa kupanda miti ili kukabiliana na athari za Mabadiliko ya tabia ya nchi.

Dkt. Jafo ameyasema hayo leo Juni Mosi,2023 Jijini Dodoma katika Shule ya Sekondari Kiwanja cha Ndege wakati akizindua wiki ya mazingira ambayo kimataifa itafanyika nchini Ivory Cost huku kitaifa ikifanyika Makao Makuu ya nchi Dodoma ikiambatana na kauli mbiu isemayo “Pinga Uchafuzi wa Mazingira unaotokana na Taka za plastiki”.

Aidha amesema kwa kipindi cha nyuma hali ilikuwa mbaya kutokana na ukame uliokua ukiyakumba baadhi ya maeneo nchini jambo lililo sababishwa na uharibufu wa mazingira.

“Lazima tuungane kuhakikisha tunatunza mazingira ndiyo maana serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt. Samia inahakikisha suala hili linatekelezwa ikiwemo upandaji wa miti,”amesema.

Ameongeza kuwa kupitia kampeini ya “Soma na mti” aliyoizindua mwaka 2022 ambayo ilikuwa ikihamasisha Kila mwanafunzi anapanda mti katika eneo lake na kuunga mkono juhudi za utunzaji wa mazingira.

Dkt. Jafo ameongeza kuwa ili kuweza kukabiliana na mabadilko ya tabia ya nchi ni kuhakikisha wanatengeneza miradi yenye kuhimili changamoto za mabadiliko hayo.

“Imani yangu kwa watanzania tunapo elekekea katika kielele cha maadhimisho haya tumuunge mkono Rais wetu kwa juhudi anazo zifanya ili kuhakikisha mazingira yanaendelea kuwa safi katika maeneo yetu,”ameongeza Dkt. Jafo.


Sanjari na hayo Waziri Jafo amemuagiza kaimu mkurugenzi wa Jiji kuhakikisha wanajenga ukuta wa fensi katika Shule hiyo na Ofisi yake imetoa mifuko 200 kwaajili ya kuanza kufyatua tofali.

“Wakati tunaendelea kusubiria ukuta wa fensi, afisa mazingira wa Jiji naomba kwanza tupate fensi ya michongoma ili tuendelee kutunza mazingira,”amesema.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amempongeza Rais Samia kwa kuendeleza juhudi za kutunza mazingira katika mkaoa wa Dodoma tangu akiwa makamu wa Rais mpaka sasa.

Amesema kuhusu suala la mifuko ya plastiki wameshirikiana na NEMC, kuhakikisha wanapambana na matumizi ya mifuko hiyo ikiwemo katika maeneo ya masoko isipokuwa katika baadhi ya maeneo bado kuna changamoto ya watu wanao tumia mifuko hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake Shadia Ramadhan Kimaro mwanafunzi wa kidato cha nne amemuahidi Waziri Jafo kuwa watahakikisha wanatunza miti hiyo walio ipanda ili kuhakikisha lengo la serikali la kupanda miti katika maeneo mbalimbali nchini linatimia.

Pia amemuomba kuwajengea uzio katika eneo la shule hiyo kutokana na changamoto wanazokutana nazo wakiwa darasani.

Kilele cha maadhimisho ya wiki ya mazingira Kitaifa itanyika Juni 5,2023 ,Mgeni Rasmi akitarakiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Mpango na yatafanyika Jijini Dodoma kuanzia eneo la Makulu kuelekea Chimwaga.









No comments