RC CHALAMILA AKUTANA NA VIONGOZI WA KAMATI YA AMANI DSM
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo Juni 6, 2023 amekutana na Viongozi wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam Ofisini kwake Ilala Boma.
Mhe Albert Chalamila amepata wasaa wa kuzungumza mambo mbalimbali na Viongozi hao miongoni mwa ajenda ni maandalizi ya Mkutano na Vingozi wa Dini wa madhehebu mbalimbali pamoja na Chakula cha pamoja na Viongozi hao wa Mkoa.
Mkutano na Viongozi wa Amani unatarajiwa kufanyika Kesho Juni 07, 2023 kuanzia Saa 3:00 Asubuhi katika Ukumbi wa PSSSF- Golden Jubilee Posta
Aidha RC Chalamila amesema lengo la Mkutano huo na Viongozi wa Dini ni kuliombea Taifa pia Kujitambulisha kwa Viongozi hao, ikiwa ni muendelezo wa utaratibu aliojiwekea toka ahamishiwe katika Mkoa wa Dar es Salaam na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan akitokea Mkoa wa Kagera.
Hata hivyo RC Chalamila ametoa rai kwa Viongozi wa madhehebu mbalimbali kuhudhuria kwa wingi katika Mkutano huo.
Kwa upande wa Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Ndg Omary Kawambwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa amewaomba Viongozi wa Dini kutoka madhehebu mbalimbali kuhudhuria kwa wingi bila kukosa Mkutano huo
No comments