Breaking News

LHRC YASHAURI KUBORESHWA VIPENGERE TATA KISHERIA MKATABA BANDARI NA DP WORLD

Mkurugenzi Mtendaji Lhrc, Anna Henga kifafanua jambo wakati akizungumza nq waandisho wa habari jijini Dar es salaam.

Dar es Salaam.
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), kimeishauri Serikali kurejea upya vipengere vyenye changamoto kisheria katikq mkataba wa bandari kati ya serikali na kampuni ya DP World ya Dubai.

Akizungumza leo Juni 13, 2023bjijini Dar es salaam, Mkurugenzi Mtendaji LHRC, Wakili Anna Henga amesema Serikali inatakiwa kurejea upya vipengele vyote katika mkataba huo vyenye changamoto ya kisheria, hususani vile vilivyoibua mijadala mikubwa kwa wananchi.

Amesema Serikali inatakuwa kuchukua hatua za haraka kufanyia maboreshi na marekebisho mapema na kuweka wazi hasa kuhusu mazingira imara ya mkataba hususani mazingira ya kikodi yaainishwe bayana ili kuepuka kutumia mwanya huo kwa maslahi binafsi na kuumiza maslahi ya umma.

"Serikali ichukue hatua za haraka kufanyia maboreshi na marekebisho mapema na kuweka wazi hasa kuhusu mazingira imara ya mkataba hususani mazingira ya kikodi yaainishwe bayana ili kuepuka kutumia mwanya huo kwa maslahi binafsi na kuumiza maslahi ya umma." Alisema Wakili Henga

Aidha LHRC Imeitaka Serikali kuweka wazi kiwango cha umiliki wa sehemu ya uwekezaji huo ili wananchi kufahamu faida itakayopatikana katika uwekezaji hususani katika mikataba ya utekelezaji wa mradi.

"Ni vema kuendelea kwa ari ya uwazi wa mikataba ya kiuwekezaji inayohusu maslahi mapana kwa Taifa kama ilivyojitokeza katika mkataba huu kati ya Serikali na Dp World," Alisema Wakili Henga.

Alisema LHRC Imeishauri serikali juu ya uwepo wa ushirikishwaji mpana wa wananchi kwani mkataba huu ambao uliopitishwa na Bunge Juni 10, 2023 haukuwa na ushirikishwaji wa kutosha.

Aidha wakili Henga aliongeza kuwa mkataba huo iainishe ukomo wa juu na chini wa motisha ya kikodi zitakazotolewa katika mikataba mingine ya utekelezaji ili kuepuka kutumika vibaya kwa kipengele hicho kwa baadhi ya watendaji wa serikali wasio waaminifu.

No comments