Breaking News

TRA WAZINDUA KAMPENI YA TUWAJIBIKE

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi Bw. Richard Kayombo wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) akifafanua jbo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampeni ya TUWAJIBIKE.

Dar es salaam:
Mamlaka ya mapato Tanzania TRA imezindua rasmi kampeni mpya ya TUWAJIBIKE kampeni ambayo imelenga kuhamasisha wafanyabiashara kutoa risiti za EFD pindi wauzapo bidhaa pamoja na wanunuzi kudai risiti pindi wanapo nunua bidhaa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mkurugenzi wa kitengo cha huduma na elimu kwa mlipakodi Bwana Richard Kayombo amesema kampeni hiyo ambayo itafanyika nchini nzima ni kuwakumbusha na kuwahamashisha wauzaji wa bidhaa na watoa huduma kuwajibika kutoa risiti halali za EFD kila wauzapo bidhaa au kutoa huduma.

"Lengo kubwa la kampeni hii ya TUWAJIBIKE ni kuwahamashisha wauzaji wa bidhaa na watoa huduma nchi nzima kuwajibika kutoa risiti halali za EFD kila wauzapo bidhaa au kutoa huduma" Alisema Bw. Kayombo.

Alisema pia kampeni hiyo imelenga kuwakumbusha na kwahamasisha wanunuzi wa bidhaa na huduma kote nchini kuwajibuka kudai risiti halali ya EFD ikiwa ni pamoja na kuzikagua ili kujiridhisha kuwa inakidhi vigezo vyote muhimu.

Amevitaja vigezo hivyo kuwa ni jina la biashara, tarehe halisi ya mauzo, kiasi halisi cha pesa kilichonunua bidhaa au huduma Jina au TIN ya mnunuzi.

kampeni hiyo itaenda sambamba na ufatiliaji wa utoaji wa risiti halali ya EFD nchi nzima pamoja na kuchukua hatua kwa wauzaji wasiofata sheria katika utoaji wa risiti halali.

Amezitaja adhabu ambazo zinaweza kutolewa kwa wale watakaobainika kutokutoa risiti halali za EFD au kufanya udanganyifu ni faini ya milioni 3 mpaka million 4 na nusu au kifungo kisichozidi miaka 3 au vyote kwa pamoja, na kwa upande wa mnunuzi ambaye atafanya manunuzi bila kudai risiti halali ya EFD atatozwa faini ya elfu 30 mpaka million 1 na nusu.

Aidha bw. kayombo ametoa wito kwa wafanyabiashara wote kuwajibika kwa kutoa risiti halali za EFD bila kushurutishwa na wanunuzi kudai risiti halali EFD  kwa kila manunuzi wanayofanya ili kuepuka usumbufu usio wa lazima hivyo kuisaidia serikali kutimiza malengo yake ya kuwaletea wananchi maendeleo na kukuza uchumi wa nchi yetu.  

No comments