Breaking News

SWIFTCABB APP KURAHISISHA HUDUMU ZA USAFIRI NA USAFIRISHAJI, WANAFUNZI WA VYUO WAPEWA MBINU ZA AJIRA

Katibu tawala mkoa wa Dar es salaam, Bi Frola Mgonja akifafanua jambo kwa maafisa usafirishaji Boda Bodo, Bajaji na guta na wanafunzi kutoka vyuo vikuu mbalimbali (hawapo pichani) katika hafla ya uzinduzi wa Swiftcabb App uzinduzi iliyofanyika katika chuo cha Utalii jijini Dar es salaam 
Mkurugenzi wa Tanswift na Swift cabb Tanzania Adv. Japhet Tesha akifafanua jambo katika hafla ya uzinduzi wa Swift cabb App uzinduzi huo iliyofanyika katika chuo cha Utalii jijini Dar es salaam
Mkaguzi msaidi kutoka Trafiki Makao Makuu dawati la elimu Insipekta Faustina Ndunguru akiwasilisha mada katika hafla ya uzinduzi wa Swiftcabb App uzinduzi iliyofanyika katika chuo cha Utalii jijini Dar es salaam.

Dar es salaam:
Kampuni ya Tanswift imezindua Swift Cabb Application ambayo inatoa  huduma ya usafirishaji mtandaoni na  inayompa fursa Afisa usafirishaji na Wanafunzi wa chuo kujipatia kipato. 

katika hafla ya uzinduzi wa Tukio hilo uliofanyika 13 May 2023 katika ukumbi wa chuo cha  utalii Jijini Dar es salaam.

Swift cabb ni application inayotoa huduma ya usafirishaji mtandaoni ambayo inamkutanisha kati dereva(Boda Boda, maguta na bajaji) na mteja kwa urahisi zaidi na gharama Nafuu. 

Uzinduzi wa Swift Cabb leo mgeni Rasmi wa tukio alikuwa Afisa katibu tawala Mkoa wa Dar es salaam Frola Mgonja na pia  iliambatana na matukio mawili ambayo ni utoaji wa elimu na mafunzo kwa maafisa usafirishaji kutoka wilaya/kanda  zote tano zinazopatika Dar es salaam na Tukio la pili wanafunzi wa vyuo vikuu wamepewa semina ya kuwa maafisa masoko ya swift cabb. 

Mgeni rasmi wa Tukio hili Frola Mgonja ameipongeza kampuni ya Tanswift kwa kuleta Swift cabb kwa wakati muafaka kwani imempa fursa ya ajira kwa vijana na imerahisisha huduma ya usafirishaji kwa kuleta gharama nafuu. 

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Tanswift Adv. Japhet Tesha amefafanua na kueleza juu ya Swiftcabb amesema ni application inayomkata makato afisa usafirishaji 15%, tofauti na makampuni mengine ya huduma ya usafirishaji mtandao ambayo wa makato ya 20%.

"kwa mujibu wa LATRA Makapuni ya huduma ya usafirishaji mtandaoni kiwango chini cha makato ni 15%, Hivyo swiftcabb ilitamani kupunguza chini ya hapo ila iwezekani" Alisema Adv. Tesha

Adv. Japhet Tesha Pia amefafanua fursa nyingine iliyopo ndani ya Swift cabb, Mteja anapata marejesha ya nyongeza kwa kila safari na ana uwezo ya kuitoa na kutumia katika matumizi mengine, Pia fursa nyingine ni wanafunzi wa chuo kikuu kapata ajira ya afisa masoko kwa kujitengenezea kipato akiwa bado anasoma. 

Naye Mkaguzi msaidi kutoka Trafiki Makao Makuu dawati la elimu  Faustina Ndunguru ameipongeza Tanswift kwa kutambua umuhimu wa kuwapa mafunzo afisa usafirishaji hao hili kila mmoja aheshimu alama na michoro ya barabarani hivyo kupitia mafunzo hayo kwa madereva hawa watakuwa mabalozi kuwaelemisha madereva wenzao, kuheshima alama na michoro ya Barabarani

No comments