Breaking News

WAZAZI NA WALEZI TAMBUENI UMUHIMU WA CHANJO

Afisa Mpango wa Chanjo Taifa kutoka Wizara ya Afya, Bi. Rotalis Gadau akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ufinguzi wa semina ya siku moja ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari juu ya umuhimu wa chanjo iliyofanyika jijini Dar es salaam.

Dar es salaam:
Wazazi na walezi nchini wametakiwa kuhakikisha watoto wao wanapatiwa chanjo zote muhimu ili kuimarisha kinga za miili yao kwani chanjo huokoa zaidi ya Vifo milioni mbili mpaka milioni tatu vya watu  hususani watoto kila mwaka.

Wito huo umetolewa leo na Meya wa Halmashauri ya Jiji la Dar es salaam Ilala Omary Kumbilamoto wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja kwa wanahabari jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa Chanjo amesema chanjo ina uwezo wa kuzuia magonjwa mbalimbali kwa mtoto hivyo kumkinga dhidi ya ugonjwa, ulemavu na hata kifo.

"Mtoto asipopatiwa chanjo ataweza kukumbwa na magonjwa ya mlipuko kama Polio, surua na rubella ambayo yanaweza kumsababishia ulemavu au hata kifo" Alisema Mhe Kumbilamoto.

Aidha Kumbilamoto ameendelea kuwasisitiza wazazi na walezi hususani wa watoto wao wakike walio chini ya miaka 14 kuhakikisha kuwa wanapatiwa chanjo ya Saratani ya shingo na mlango wa kizazi.

Kwa upande wake Afisa Mpango wa Chanjo Taifa kutoka Wizara ya Afya, Bi. Rotalis Gadau amesema kuanzia mwaka 2019 mpaka 2020 kiwango cha huduma za chanjo kiliongezeka kwa kiasi kikubwa kwa takribani asilimia 95% ambapo kwa mwaka 2020/2021 kiwango kilishuka na kufikia asilimia 81% kutokana na Mlipuko wa Ugonjwa wa Virusi vya Korona UVIKO-19.

"Baada ya mlipuko wa Uviko-19 Watu wengi waliogopa kufika kwenye vituo vya Afya ili kupata Chanjo wakihofia watoto wao na wao wenyewe kupata UVIKO-19" Alisema Bi. Gadau.

Amebainisha kuwa kutokana na Mdororo huo wa mwitikio wanajamii kuwachanja watoto wao mwaka 2022 kuliibuka mlipuko wa ugonjwa wa surua na Watoto Takribani 3,923 walibainika kupata ugonjwa huo.

Bi. Gadau aliongeza kuwa Mpango wa Taifa wa Chanjo umekuwa ukihakikisha wanajiunga na Kampeni nyingine za Afya ikiwemo, kampeni ya HIV, Malaria na RCH  ili kutoa Elimu ya chanjo na chanjo.

No comments