Breaking News

JESHI LA POLISI KUSHIRIKIANA NA CHUO CHA UDSM KUFANYA UTAFITI

Na mwandishi wetu Jeshi la Polisi- Dar es salaam.
Jeshi la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na mabadiliko ya sayansi na technolojia limepanga kuja na mkakati wa Pamoja kwa kushirikiana na chuo kikuu cha Dar es salaam katika maswala ya tafiti mbalimbali ambazo zimelenga kubaini na kukomesha vitendo vya kiharifu.

Akiongea na waandishi wa Habari mkuu wa chuo cha taaluma ya Polisi Dar es salaam kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi SACP Dr. Lazaro Mambosasa amesema moja ya majukumu yao ni kulinda rai ana mali zao ambapo amebainisha kuwa kupitia kitengo cha utafiti ndani ya Jeshi hilo na katika chuo cha Taaluma ya Polisi Dar es salaam wameona vyema wafike chuoni hapo ili kujifunza maswala mbalimbali katika tafiti.

Aidha SACP Dr. Mambosasa amewambia waandishi kuwa malengo ya Mkuu wa Jeshi hilo IGP Camillus Wambura ni kuona Jeshi la Polisi linawekeza katika tafiti ambapo amebainisha kuwa Jeshi hilo limepanga kuingia makubaliano baina ya chuo cha taaluma ya Polisi Dar es salaam Pamoja na chuo kikuu cha Dar es salaam katika kufanya tafiti.

Nae Kamishina Msaidizi wa Polisi ACP RALPH MEELA ambae ni  Mkuu wa Kituo cha Utafiti cha Jeshi la Polisi kilichopo Chuo cha Taaluma ya Polisi Dar Es Salaam amesema kuwa kutokana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia wameona vyema waje na mtazamo mpya katika kutanzua mbinu zinazotumiwa na wahalifu. 

No comments