Breaking News

HIZI HAPA FILAMU 88 ZILIZOCHAGULIWA NA ZIFF 2023

Mkurugenzi Mtendaji wa ZIFF Prof Martin Mhando akionesha bango la Tamasha la mwaka huu wakati wa kutangaza filamu zilichaguliwa mwaka huu.

NA ANDREW CHALE - DAR ES SALAAM.
TAMASHA la Kimataifa la la filamu za Nchi za Majahazi (ZIFF) limetangaza rasmi filamu 88 zilizochaguliwa  mwaka huu ambazo zitaoneshwa katika viunga vya Unguja, Zanzibar. 

Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa ZIFF, Prof Martin Mhando amesema mwaka huu limebeba mada ya 'KUJITAMBUA'.

"Kwa kutambua utashi wa mwanadamu kwenye mawasiliano,  tulitembelea Michoro ya Mapangoni ya Kolo iliyoko Kondoa,  niligundua kipengele muhimu cha utashi wa binadamu-mawasiliano, hivyo bango letu limebeba Michoro ya kolo kama kujitambua". Amesema Prof Martin Mhando.

Prof.Martin Mhando amebainisha kuwa, filamu nyingi zimeweza kutumwa lakini wameweza kuchagua filamu hizo 88 ambazo zimeonekana nzuri zaidi ya zingine.

Amezitaja filamu hizo kuwa:
Upande wa filamu ndefe (Features films) zipo 18 ambazo ni: Bounty kutoka nchi ya Switzerland,
L.I.F.E. (Nigeria),
Twin flame (USA/Nigeria),
Wandongwa (Tanzania),
Samara (Spain),
Still Okay to date?(Tanzania),
Soudabeh(Iran),
Whenever I am alone with you (Ufaransa).

Citizen Kwame (Rwanda)
When the levees broke (Cameroon)
Wounded Psyche (Iran),
Mister Sister (Canada-USA),
Dodoma (Tanzania),
Married to work (Kenya)
Gereza (South Africa)
Behind gates(Cameroon)
Half open window (Kenya),
Rat hole (Egypt) na zingine. 

Kwa upande wa filamu fupifupi (short films 45) ni: 
The Letters (Ireland),
DEEP (South Korea),
THE MIST (South Korea)
MOKSA’S FREEDOM (Indonesia), KITENDAWILI (Tanzania),
GROGAN’S LODGE (Kenya).

SWETA (Tanzania)
One day plus enternity (Iran),
JASIRI (Tanzania),
Hummus and Chips (Egypt),
Flesh and blood (Tunisia),
Light blue (Egypt),
RE-CASTED (Iraq),
Cobbler of Paradise (Iraq),
Neb tawy (Egypt),
The Moped and Goldfinch (Algeria),
Na ZONGI (Angola),
9 Memeza (South Africa)
Epiphany (United States),
Under the bed/chini ya chaga (Tanzania),
ZIWA (Uganda),
LAILA (Saudi Arabia),
The shoes that get smaller every night (Bahrain),

FRAIHA (Qatar),
Laugh lines (Bangladesh)
Act of love (Kenya),
Seven stages (South Africa),
Supastaz (Kenya),
A beautiful Mess (South Africa)
Talk to me (Kenya)
The broken mask (Nigeria),
In the stillness (Nigeria),
A Void life (Uganda),
Our territories, our voice (Kenya),
Ngozi nyeusi (Tanzania)
I believe in me (Tanzania)
NIA (Tanzania),

MWANDISHI / WRITER (Tanzania) na zingine. 

Upande wa filamu makala  (Documentaries) jumla zipo 24:

The Fisherman's net (Germany),
Untitled Baltimore  documentary (United States)
Voice of Pemba (Kenya),
The Zanzibar plan (Canada),
Upstanding (Rwanda),
Apostles of cinema (Tanzania) na nyingine nyingi.


No comments