Breaking News

DAR ES SALAAM YANG'ARA MWENGE WA UHURU 2023

Dar es Salaam:
Mwenge wa Uhuru 2023 Mkoa wa Dar es Salaam ukiongozwa na Ndg Abdallah Shaib Kaim kutoka Mkoa wa kaskazini pemba (Kiongozi) umekimbizwa katika umbali wa KM 499.9 kwa kupitia miradi 32 kwa mchanganuo wa Wilaya ya Temeke miradi 6, Kigamboni miradi 6, Ilala miradi 6, Ubungo miradi 7 na Kinondoni miradi 7 yote ikiwa na thamani ya Tsh 93,457,467,363.83/=

Aidha Wananchi wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa pamoja wameungana na Watanzania wote katika kupokea ujumbe wa mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 unaosisitiza umuhimu wa kuhifadhi mazingira, Vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe hai, na Uchumi wa Taifa chini ya kauli mbiu isemayo " Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe hai na Uchumi wa Taifa "

Vilevile Mwenge wa Uhuru umehamasisha wananchi kuendeleza Mapambano dhidi VVU/ UKIMWI, Malaria, Dawa za kulevya, Lishe na Rushwa

Sambamba na hilo Mwenge wa Uhuru 2023 kila ulipo pita umehamasisha shughuli mbalimbali za maendeleo, Upendo, Amani, Mshikamano na uzalendo kwa Wananchi

Ifahamike kuwa Mwenge huo katika Mkoa wa Dar es Salaam  ulipokelewa ukitokea Mkoa wa Pwani Mei 24, 2023  umekimbizwa katika Wilaya zote 5 za Mkoa hadi Mei 28, 2023 ambapo unatarajiwa Kukabidhiwa Mei 29, 2023 Kusini Magharibi- Zanzibar na Mkuu wa Mkoa Mhe Albert J Chalamila.



No comments