ACT WAZALENDO WAITAKA JAMII KUWALINDA WATOTO NA KUWA NA VIONGOZI IMARA KWA MASLAHI YA TAIFA
CHAMA cha ACT-Wazalendo kimetoa wito kwa jamii kuhakikisha watoto wanalindwa ili kufikia malengo yao sambamba kuwa viongozi imara kwa maslahi ya taifa.
Hayo yamesemwa leo na Dorothy Semu Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho Tanzania-Bara alipokuwa katika kituo cha kulea watoto yatima cha Sara House kilichopo Mwandege wilayani Mkurunga ,Mkoa wa Pwani.
Dorothy akiwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa wa chama hicho pamoja na Janeth Rithe Naibu Katibu wa Uenezi , Bonifacia Mapunda Katibu wa Ngome ya wanawake, Sevilina Mwijage Mjumbe wa Halmashauri Kuu, na Mwenyeji wao Mohammed Mtambo Katibu wa ACT-Pwani,na wanachama wengine waandamizi wa Chama hicho.
Dorothy amesema kuwa kuwalinda watoto ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanakuwa salama kisaikolojia na kimwili ili kupata viongozi imara watakaoliongoza taifa .
"Suala la ulinzi wa watoto ni wajibu wetu sote ,kila mtu ahusike katika kumlinda mtoto wa Kitanzania ili kuhakikisha watoto wetu wanakuwa salama na kuepushwa madhara yakisaikolojia ,au kimwili ", Dorothy.
Amesema kuwa ripoti za haki za Binadamu ha mwaka 2022, ilionyesha kuwa matendo ya unyayasaji watoto yameongezeka na kwamba hali hiyo haina ustawi mzuri wa watoto.
IMETOLEWA LEO
04 /5/ 2023
JANETH JOEL RITHE
N/KATIBU MWENEZI
No comments