Breaking News

TAASISI YA MAMA ONGEA NA MWANAO YATOA MKONO EID KWA VITUO VYA WATOTO YATIMA KINONDONI

Mwenyekiti wa Taasisi ya Mama Ongea na Mwanao bwana Steven Mengele maarufu (Steve Nyerere) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari mara baada ya wakikabidhi msaada wa vitu mbalimbali kwa vituo vya lulelea watoto wahishio katika mazingira magumu jijini Dar es Salaam.

Dar es Salaam:
TAASISI ya Mama Ongea na Mwanao katika kipindi hiki cha mfungo Mtukufu wa Ramadhani imetoa msaada wa vitu mbalimbali kwa watoto yatima wa Wilaya ya Kinondoni.

Akizungumza leo Aprili 19, 2023 jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi vitu hivyo Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Steven Mengele arimaarufu Steve Nyerere amesema lengo ni kuwashika mkono watoto hao.

Mengele amesema katika kipindi hiki cha mfungo Mtukufu wa Ramadhani wamekuwa wakiwashika mkono yatima kwa kuwafutulisha, lakini wao wameamua kuwashika mkono kupitia msaada huo.

Mengele ametaja vitu hivyo walivyokabidhi kuwa ni pamoja na hijabu 500, michele, mafuta na misahafu.

“Leo hapa tumekuja kuwashika mkono watoto yatima wa Wilaya ya Kinondoni, na msaada huu tunautoa kwa vituo vitatu, ambavyo ni Faraji, Chakuwama na Upendo Center,” amesema Mengele.

Pamoja na msaada huo Taasisi hiyo imemshika mkono Mama Mzazi wa Msanii wa Vichekesho nchini Zimwi kwa kumpatia zawadi kutoka kwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Vile vile imemkabidhi michele, mafuta na kumhakikishia kwamba wapo pamoja naye kuhakikisha mwanaye anarudi katika hali nzuri kiafya na kurejea katika shughuli zake.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni Songoro Mnyonge ameipongeza Taasisi hiyo kwa kufanya jambo hilo zuri.

Katika hatua nyingine Mengele amekemea kitendo alichofanya Mwenyekiti wa Ngome ya Vijana wa ACT Wazalendo Abdul Nondo cha kuhamasisha maandamano.

No comments