Breaking News

FRIENDS OF SAMIA WAFUTURISHA MAYATIMA

Dar es Salaam;
Wasanii Ali Kiba, Tommy Flavor , MauaSama na Marafiki wengine wa Samia wametoa sadaka kwa kufuturu na mayatima wanaolelewa katika kituo cha IJANGO ZAIDI ORPHANAGE CENTRE kilichopo Sinza jijini Dar es Salaam.  

Sambamba na hilo marafiki hao wa Samia wametoa mahitaji mbalimbali katika kituo hicho na kuahidi kuendelea kuwa walezi kwa kipindi chote.

 Wasanii Alikiba na Maua Sama pamoja na watangazaji Mwijaku na Geah Habib wamefika katika Iftar iliyoandaliwa na Friends of Samia (Marafiki wa Mhe. Rais Samia) katika kituo cha kulea watoto Yatima na wenye uhitaji cha Ijango kilichopo Sinza, Dar es Salaam.

Sambamba na Iftar hiyo, pia kundi hilo limetoa zawadi ya mahitaji tofauti tofauti hasa chakuka kwa watoto hao na kuwapa furaha kwa niamba ya Mhe, Rais Samia Suluhu Hassan.








No comments