Breaking News

MAANDALIZI KUELEKEA PAMAMBO KATI YA MWAKINYO Vs KETEMBO YAMEKAMILIKA KWA ASILIMIA 100


Maandalizi ya pambano linalosubiliwa kwa hamu na wapenzi na wadau wa mchezo wa ngumi nchini lililopewa jina la FIGHT with PURPOSE kati ya bondia Hassan Mwakinyo Vs Kuwesa Ketimbi 
yamekamilika kwa asilimia 100 pambano ambalo linatarajiwa kufanyika 24 April katika uwanja wa jamhuri jijini Dodoma

Pambano hilo lililoandaliwa na kampuni ya Lady in Red litakuwa pia na mapambano ya awali kutoka kwa baadhi ya wabunge wa bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania ambao watapamda jukwaani kuzichapa katika mapambano ya round mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolea kwa vyombo vya habari imesema kuwa maandalizi kuelekea pambano hilo yamekamilika kwa asilimia 100 hivyo kuwataka wapenzi na wadau wa mchezo huo kujitokeza siku ya pambano hilo 24 April katika viwanja vya Jamhuri Dodoma.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa Viingilio siku ya pambano hilo vitakuwa ni VIP B-20,000, VIP B 100,000, VVIP 300,000 wakati kawaida itakuwa 10,000 

Tiketi za pambano hilo zinapatikana katika ofisi zote za TTCL nchi nzima, Mawakala wa N-Card, Mawakala wa NBC, Mawakala wa CRDB, N-Card APP, Vunja bei barabara ya 7 poja na uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.


No comments