Breaking News

DKT. MWINYI ASEMA AMANI NI FAIDA KWA MUUNGANO

Zanzibar:
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Tanzania inajivunia   Muungano wa Tanganyika na Zanzibar kama mfano barani Afrika. 

Ameyasema hayo leo tarehe 25 Aprili alipohutubia Kongamano la Miaka 59 kuadhimisha  Muungano wa Tanzania lililofanyika ukumbi wa Idris Abdul-Wakil Kikwajuni, Mkoa wa Mjini Magharibi. 

Amewashukuru watoa mada wa Kongamano hilo, Profesa Patrick Loch Otieno  Lumumba kutoka Kenya kwa mada ya umuhimu wa Muungano na umoja katika bara la Afrika na Waziri mstaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mzee Stephen Wassira  kwa kuwasilisha mada ya historia ya umuhimu wa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar pamoja na Mhe.Balozi Mohamed Hamza  mada yake ikijikita katika fursa zilizopo kwa vijana ndani ya Muungano.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema kuwepo kwa amani kwa taifa  ni faida mojawapo ya Muungano  kwa maendeleo alibainisha kuwa   awamu zote zilizopita za  utawala mpaka sasa zimekuwa  zikidumisha uhusiano mwema, utamaduni, lugha   fursa nyingi  za ajira  ushiriki wa siasa  na kutumia rasimali zilizopo kwa pande zote mbili za Muungano.




No comments