Breaking News

USAHIHI WA UTABIRI WA HALI YA HEWA UNAOTOLEWA NA TMA WAFIKIA 88.5 %

Imeelezwa kuwa viwango vya usahihi wa utabiri wa hali ya hewa unaotolewa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini –TMA kwa ujumla vimeongezeka na kufikia asilimia 88.5, ambapo katika msimu wa mvua za Vuli 2022, viwango vya usahihi vilikuwa asilimia 94.1.

Kwa mujibu wa taarifa ambayo imetolewa na Mamlaka hiyo kuhusu mafanikio ya kipindi cha miaka miwili ya uongozi wa serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan,imesema hiyo inatokana na huduma za hali ya hewa nchini kueendelea kuboreshwa na kuimarishwa katika maeneo mbalimbali ili kukidhi mahitaji ya watumiaji Kitaifa na Kimataifa.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa viwango hivyo ni juu ya kiwango cha usahihi wa utabiri kinachokubalika na Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO) cha asilimia 70 ambapo ongezeko hilo la usahihi wa utabiri unazifanya huduma za hali ya hewa zinazotolewa nchini kuwa za uhakika na kuleta mchango mkubwa katika maendeleo ya sekta zote za kiuchumi na kijamii nchini zinazotegemea hali ya hewa.

Mamlaka hiyo imesema itaendelea kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) katika kutekeleza majukumu ya sekta ya hali ya hewa kwa shughuli za utunzaji wa mazingira ikiwemo kufuatlia mabadiliko ya hali ya hewa yanayopelekea  ya Taifa letu.

No comments