Breaking News

MFAUME MFAUME KUZICHAPA NA IDDI PIALARI LIVE TENA

Pambno la marudiano la mabondia mahasimu Mfaume Mfaume kutoka Mabibo na Iddi Piarali wa Manzese linatarajiwa kufanyika Septemba Mosi mwaka huu katika Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

Pambano hilo la maeudiano linaua kufatia pambano la awali kuvunjika baada ya kugongana vichwa kulikopelelea Piarali kupata jeraha juu ya paji la uso na kusababisha kutoka kwa damu nyingi kitendo kilichosababisha pambano hilo kukatika.

Akizungumza wakati wa zoezi la kusaini mkataba wa pambano hilo lililopewa jina la "King of the Night" Promota Khamisi Mrisho amesema mabondia hao siku hiyo watawania mkanda wa Ubingwa wa (WBF) uzito wa kati pambano la raundi 12.

Alisema lengo la kurudia kwa pambano hilo ni kutafuta mbabe wa Dar es Salaam na bingwa wa WBF.

“Wadau na mashabiki wa mabondia wategemee kushuhidia live kurudiwa kwa pambano hilo litakalowakutanishamahasimu hao kutoka jijini Dar es salam Septemba mosi mwaka huu."Alisema Bw.Mrisho

Mapema akizungumza mara baada ya kusaini mkataba wa pambao hilo Bondia Idd Piarali amesema kuwa anatarajia kuingia kambini hivi karibuni tayali kwa kujiandaa na pambano hilo.

“Watanzania, wapenzi wa mchezo wa ndondi na mashabiki wangu wategemee burudani kutoka kwangu, dua zanu ni muhimu ili niwe na nguvu na afya nzuri mimi pamoja na mpinzani wangu Mfaume Mfaume,” Alisema Piarali.

Kwa upande wake Bondia Mfaume Mfaume amewataka wadau na mashabiki zake wategemee ushindi wa mapema, kutokana na mazoezi anayoendelea kuyafanya.

"Mashabiki na wadau wangu tegemeeni ushindi tena ushindi wa mapema tu kufatia mazoezi makali nayofanya kuelekea siku hiyo ya pambano letu September mosi mwaka huu" Alisema Bondia Mfaume

Pambano lao la awali Lililofanyika Disemba 25, 2022 Kamisheni ya ngumi za kulipwa Tanzania (TPBRC) walivunja kutokana na mpinzani wake, Piarali kupata jeraha juu ya paji uso hivyo pambano la marudiano mashabiki wanahitaji matokeo ya kweli.

No comments