Breaking News

WANAHABARI WAPIGWA MSASA JUU YA MAGONJWA WA TB NA KIFUA KIKUU

Tanzania ya nchi ambayo inatajwa kuwa miongoni mwa nchi 30 Duniani zenye wagonjwa wengi wa TB ambazo huchangia asilimia 87 ya Wagonjwa wote Duniani (Takwimu za shirika la Afya Duniani (WHO)wa Mwaka 2021) .

Akiwasilisha mada katika semina ya kuwajengea uwezo waandishi waandamizi kutoka vyombo mbalimbali vya habari Mratibu wa Kifua Kikuu na Ukoma kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Dokta Mbarouk Seif takwimu zinaonyesha kuwa takribani watu 132,000 waliugua ugonjwa huo nchini.

Amesema kwa mwaka 2021 Tanzania ilikadiriwa kuwa na wagonjwa wapatao 132,000 waliougua Kifua Kikuu, ikiwa ni sawa na uwiano wa wagonjwa 208 kwa kila jamii ya watu 100,000 ambapo wagonjwa 87,415 sawa na asilimia 65 waligundulika.

“Takwimu zinaonyesha kuwa asilimia 35 ya wagonjwa hawakuweza kufikiwa na kuwekwa kwenye matibabu hivyo kuendelea kuwaambukiza watu wengine katika jamii, ni jukumu letu kuendelea kuwatafuta kwa kila hali na kuwaweka katika matibabu Ili kupunguza maambukizi ya kifua Kikuu katika Jamii’ Alisema Dkt. Seif

Aidha dkt. Seif aliongeza kwa mujibu wa takwimu Jiji la Dar es Salaam lina jumla ya wagonjwa wapatao 5414 ambao waliweza kuikuliwa na kuwekwa kwenye tiba mwaka 2022 ambayo ni sawa na asilimia 102 ya lengo la uibuaji 5311.

Nae Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri Jiji la Dar Es Salaam Dkt ,Reginard Mlay alisema ukiwa na Afya njema utafanya kazi zako vizuri na Uchumi wa nchi utakuwa .

Alisema kila Mwaka kama taifa tumekuwa tukiadhimisha siku hiyo kwa lengo la kuweza kufikisha ujumbe kwa jamii kuanzia ngazi ya kaya, mitaa, Kata,Wilaya mpaka Mkoa dhumuni kupeana elimu Ili ujumbe ufike kwa jamii kwa ajili ya mapambano ya Kifua Kikuu .

Kwa upande wake Mjumbe wa Bodi ya Tanzania stop TB Partnership Bi. Agatha Mshanga alielezea umuhimu wa wanahabari katika kudhibiti Kifua Kikuu nchini kutokana na mchango wao mkubwa kwa jamii hasa katika kutoa elimu kuhusiana na Kifua Kikuu.

"Waandishi wa habari mnao wajibu wa kuandaa habari na Makala mbalimbali, kutoa elimu kwa jamii kuhusiana na ugonjwa huo na dhana potofu juu ya ugonjwa huo wa Kifua Kikuu na kuelimisha kwamba ugonjwa wa Kifua Kikuu unatibika, kupona na pia unaweza kuzuilika" Alisema Bi. Mshanga

Mapema akiwasilisha mada katika washa hiyo Mratibu wa TB kutoka Tanzania STOP TB Partnership Bwana Nelson Telekera alisema madhimisho ya Kifua Kikuu ambayo mwaka yanataraji kufanyika Mkoani.

Maadhimisho ya siku ya  Kifua Kikuu na Ukoma ambayo yatafanyika Machi 24 ambayo yamepewa Kaulimbiu ya “Kwa pamoja tunaweza kutokomeza Kifua Kikuu nchini Tanzania“ mgeni Rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa. 


No comments