CHAUMMA KUTEMBEZA BAKULI KUOMBA FEDHA ZA KUENDESHA MIKUTANO YA HADHARA,WAMPA PONGEZI RAIS SAMIA
Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA, Hashim Rungwe Spunda akifafanua jambo mara baada kikao cha Kamati kuu ya chama hicho jijini Dar es salaam.
Dar es salaam:
Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) kimewaomba wadau na wanachama wa chama hicho kukichangia chama ili kufanikisha mikutano yake ya hadhara ambayo inatarajiwa kuanza mwishoni mwa mwezi Machi mwaka huu wa 2023.
Akizungumza makao makuu ya chama hicho jijini Dar es Salaam mwenyekiti taifa wa Chama hicho Taifa, Hashim Rungwe Spunda mara baada ya kalizika kwa kikao cha Kamati kuu ya chama hicho.
Rungwe amesema kwa sasa chama hakina pesa za kutosha za kuendesha mikutano yao nchi nzima hivyo wanatarajia kufanya mikutano yao ya awali kwa kuwafuata wananchi katika maeneo yao ya shughuli ikiwemo maeneo ya masoko na stedi za mabasi.
"Tunawaomba wadau,mashabiki na wanachama kukichangia chama kupitia akaunti zetu za CHAUMMA kwani kwa kufanya hivyo kutawezesha kufanikisha kufanya kampeni zetu na kutoa sera za chama na kuainisha mapungufu ya Serikali inayotutawala ambayo inaongozwa na CCM"alisema Hashim Rungwe.
Mbali na hayo kupitia kikao hicho kimewapongeza Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Alli Mwinyi na Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza majukumu yao ipasavyo huku wakitumia nafasi hiyo kumtaka Rais Samia kukubali mialiko kutoka vyama vingine vya upinzani.
"Tunampongeza Rais Samia kwa kuhudhuria mkutano wa baraza la Wanawake wa Chama cha Chadema (BAWACHA) kwani ni kitendo cha kihistoria ambacho hakijawahi kufanywa hapa nchini na ni kitendo.
No comments